Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Naura, Ndugu Sunday G.
Mshobozi ambaye pia ndiye mwalimu pekee wa somo la Fizikia kuanzia kidato cha
kwanza mpaka cha nne.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari ya Naura,
Ndugu Mary Shirima akifanya mahojiano na mwandishi kufahamu changamoto
zinazoikabili shule hiyo
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo wakiwa
katika muda wa mapumziko
Uchunguzi
uliofanywa na Shirika la HakiElimu umegundua kuwa Shule ya Sekondari ya Naura
iliyoko katika kata ya Lemara , eneo la Njiro ni miongoni mwa shule zenye maendeleo
hafifu ya kielimu ukilinganisha na shule nyingine za serikali na kata zilizoko
katika Manispaa ya Wilaya ya Arusha.
Shule
hii iliyoanzishwa mwaka 2008 , inakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu kwani
kuna masomo hayajawahi kuwa na walimu toka shule hiyo ianzishwe mfano
masomo ya Chemistry, Mathematics na Book- Keeping . Pia kuna masomo
ambayo yana mwalimu mmoja mmoja mfano English, Commerce, Literature, na
Civics toka kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Tofauti
na shule nyingine ambazo hukimbiwa na walimu kutokana na kuwa mazingira magumu
shule hii iko eneo zuri na maarufu waishio watu wenye kipato cha juu mkoani
Arusha lijulikanalo kama Njiro na kuacha maswali kuwa kama kuna tatizo la
uongozi wa shule au kuna tatizo la upangaji wa walimu unaofanywa na serikali ,
hili hali shule nyingine zikiwa na walimu lukuki.
Akielezea
sababu nyingine za kudorora kitaaluma shuleni hapa Mwalimu Mshobozi alisema
kuna mrundikano mkubwa wa wanafunzi kushinda uwezo wa shule akitolea mfano
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka huu
kufikia 307. Tofauti na malengo ya shule ya kata kusomesha wanafunzi wa maeneo
ya karibu , wanafunzi wa shule hii wanatoka katika kata zote zilizoko
manispaa hii kukiwa na umbali mrefu na kukabiliwa na shida kubwa ya usafiri
jambo ambalo pia alilielezea kuwa ni moja ya sababu za kudorora kitaaluma
kwa wanafunzi wa shuleni hapo.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi Bi Mary Shirima alisema sababu za kudodora
kitaaluma kwa shule yake ni mwako mdogo wa kielimu kwa wazazi pamoja na watoto
wenyewe akisema wengi wa wanafunzi ni kama wamelazimishwa kuja kusoma shuleni
hapo na wazazi wao hawajishughulishi na maendeleo ya watoto wao. “
Historia ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne ni tata kwani kuna waliokuwa
wameolewa na wafanyabiashara mara baada ya kumaliza darasa la saba ,ghafla
wakasikia wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kulazimika kuja
shuleni, sasa katika hali hiyo unatarajia nini” aliuliza Mwalimu Shirima.
Katika
mtihani wa kidato cha nne wa taifa wa mwaka jana 2011 jumla ya wanafunzi 164
walifanya mtihani huo ambapo hakuna aliyepata daraja la kwanza wala la
pili, wanafunzi 2 walipata daraja la tatu , 24 wakapata daraja la nne na 138
walifeli kwa kupata zero. Shule hii ilishika nafasi ya mwisho kati ya shule 137
zilizofanya mtihani huo katika mkoa wa Arusha. Kitaifa ilishika nafasi ya 2994
kati ya 3108 zilizofanya mtihani huo.
No comments:
Post a Comment