Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.
Baba mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.
Baada ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia, Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.
No comments:
Post a Comment