Leo ni ufunguzi wa rasimu ya katiba mpya na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema kwamba Rasimu hiyo imependekeza kwamba matokeo ya rais yahojiwe mahakamani.
Kwa lugha nyingine ni kwamba katiba ijayo itaruhusu Rais kushtakiwa mahakamani endapo matokeo yake yatatiliwa shaka na wagombea wengine.
Jaji Warioba ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya katika tukio la kihistoria nchini Tanzania.
"Imependekezwa kwamba matokeo ya Rais yatashikiwa mahakamani lakini kwa masharti," amesema Jaji Warioba hivi punde.
Jaji Warioba ametaja masharti hayo ni kwamba wagombea wa urais ndio watakuwa na haki ya kuhoji matokeo ya rais na si vinginevyo. Pili, matokeo hayo yanatakiwa kuhojiwa ndani ya mwezi mmoja tu na si vinginevyo.
Amesema pia tume imependekeza kuwapo kwa wabunge wa aina mbili ambao ni wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wengine wa kuteuliwa na Rais.
Pia amesema kwamba kutakuwapo kwa utaratibu wa wanawake kugombea katika majimbo. Kwa maana hiyo hakutakuwapo wabunge wa Viti Maalumu.
Pamoja na hayo, tume ya jaji Warioba imependekeza kuwepo kwa serikali tatu ambazo ni -serkali ya zanzibar, ya tanganyika na ya muungano.
mambo ya muungano yaliyopendekezwa:
1)katiba ya jamhuri ya muugano wa tanzaia
2)sarafu na benki kuu
3)mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
4)ushuru
5)ulinzi na usalama
6)usajili wa vyama vya siasa
7)uraia na uhamiaji
No comments:
Post a Comment