Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania
Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa
uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu
watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa
wamevunjika miguu.
atika Mkutano huo walikuwapo pia
Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema
sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati
nzuri Mbowe na Lema hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.
Mlipuko
huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara
tu baada ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu
kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya
watu, hali inayoashiria mrushaji huenda alilenga kuwajeruhi viongozi
hao.
Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt
Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa
na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao
kuuawa.
Hali ikiwa bado tete viwanjani hapo, magari kadhaa ya askari polisi yalifika huku askari wakiwa na silaha lakini walilazimika kupiga mabomu ya machozi kadhaa hewani na kisha kuondoka kutokana na baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira kuwafuata na kupaza sauti wakitaka wawaue pia.
Kijana mmoja muuza machungwa aliieleza blogu hii kuwa aliyerusha bomu hilo alitokea upande wa nyuma ya jukwaa kuu na badae kukimbilia nyumba zilizojirani.
No comments:
Post a Comment