Washiriki wa mashindano ya Mercedes Cup 2012 ya Boti zinazokwenda na
Upepo (Sailing Boat) wakiwa wamekusanyika Yatch Club jijini Dar kabla ya
kuanza mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors
yanayofanyika kila mwaka.
Pichani ni Boti zinazotumika katika mashindano hayo.
Washiriki wakianza mashindano hayo kuzunguka fukwe karibu na kisiwa cha Bongoyo.
Washiriki wakichuana.
Boti iliyombeba Refarii wa mashindano hayo pamoja na wasimamizi wengine.
Tuzo za washindi zikiwa mezani.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed(katikati) akijadili jambo na
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) pamoja
Catamaran Representative wa Dar es Salaam Yatch Club Andrew Boyd.
Washiriki na familia zao wakisubiri kuanza kwa zoezi la kutoa zawadi.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimkabidhi zawadi Refarii wa mashindano hayo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (Kulia) na Mkurugenzi wa
Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) katika picha ya pamoja
ya washindi wa kwanza hadi wa tatu walioshiriki mashindano ya Boti
zinazokwenda kwa upepo (Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 baada ya
kukabidhiwa vikombe na zawadi zao yaliyofanyika katika fukwe za Yatch
Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo
yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Washindi wa tatu David na Sarah Scott wakipokea zawadi na tuzo.
Katika picha ya kumbukumbu na wadhamini wa mashindano CFAO Motors.
Pichani Juu na Chini Washindi wa pili Paul na Kim Troll wakipokea zawadi kutoka CFAO Motors.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akikabidhi Kombe kwa timu ya
washindi wa kwanza wa mashindano ya Boti zinazokwenda kwa kutumia upepo
(Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 Al Bush na Jeppe yaliyofanyika
katika fukwe za Yatch Club Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh. Mashindano hayo
yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akigawa Champagne kwa washindi.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (katikati)
akizungumza machache baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo
amewataka watu kujitokeza kwa wingi kila mwaka na kutoa shukrani zake
kwa wote walioshiriki kufanikisha mashindano hayo. Kushoto ni Meneja
Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed na kulia ni Andrew Boyg wa Dar es
Salaam Yatch Club.
Mshindi wa kwaza akifungua Champagne.
Tuesday, August 14, 2012
TAIFA STARS YAWAFUATA WABOTSWANA LEO
Washambuliaji wa timu ya taifa, (Taifa Stars) Mrisho Ngassa (kulia) na
Haruna Moshi Boban wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya kwenda
Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho
Jumatano.
Nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars Juma Kasseja akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho Jumatano .
Wachezaji wa timu ya Taifa,Taifa Stars wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya safari ya kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho Jumatano.

Mgogoro wa Ziwa Nyasa na tamaa ya Malawi katika mafuta na gesi

Wanafunzi wakivuka ziwa Nyasa kuelekea shule.
SASA ieleweke wazi kwamba hali si shwari kati ya Tanzania na Malawi. Pengine ni vizuri kujiuliza leo ni kwa nini mtafuruku uchukue nafasi kubwa leo. Kivipi Mtanzania wa kawaida, aoneshwe kama ni jambo lililokuja ghafla?
Kimsingi, mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi umekuwapo kwa zaidi ya nusu karne. Hivi sasa umechukua sura mpya baada ya nchi hiyo jirani kusema ndiyo inayomiliki sehemu yote ya ziwa hilo.
Pengine kauli hiyo peke yake, isingeleta shari. Alama ya hatari imetokana na kauli ya vitisho, iliyotoka Serikali ya Malawi kwamba itafanya kila linalowezekana, ikiwamo kutumia nguvu za kijeshi kuhakikisha ziwa hilo linabaki kwenye himaya yao.
Picha iliyopo ni kwamba Malawi wameshaona Watanzania ni wapole. Kwamba ni waoga wa kupitiliza, kwa hiyo wakiambiwa kuhusu nguvu ya kijeshi, watarudi nyuma. Sijui uthubutu huu wameupata wapi lakini ninachowaza ni kwamba viongozi wa Malawi, wanahisi sisi ni mazezeta.
Vile ambavyo madai yao yalivyo hayana msingi na hayakubaliki hata kidogo, ndivyo ambavyo ukitafakari wanachokitaka kiwe, huku wakitoa vitisho vya kupigana vita, unaweza kujiuliza kuhusu wigo wa uelewa wao. Ni rahisi kuamini ndugu zetu hao wana dosari za kiufahamu.
Kweli Ziwa Nyasa lote ni lao? Huo mpaka ni wa namna gani hasa, kiasi kwamba eti Mtanzania akikanyaga tu maji ya ziwa hilo, anakuwa yupo Malawi. Muda wa kutafuta maelewano hawataki, wanakimbilia kwenye vita. Malawi wanahitaji kuwaheshimu Watanzania. Ni ukweli ulio wazi kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Malawi kutoa madai hayo, lakini ni mara yake ya kwanza kutumia kauli yenye vitisho vya kiwango hicho kinachoashiria vita kati ya Tanzania na wao. Madai hayo yalitolewa kwa mara ya kwanza na Rais wa Kwanza wa nchi hiyo, Dk. Kamuzu Banda.
Madai hayohayo, yalirudiwa na wanasiasa mbalimbali, akiwemo mmoja wa viongozi wa vyama vya upinzani, Chakufya Chiana. Baadhi ya maswali yanayoulizwa ni haya yafuatayo;
Chukua dakika mbili tu Kusoma Hii Kutoka Gazeti la Uwazi "INASIKITISHA"
Taarifa zilizopenyezwa na ndugu mmoja wa Simon Sakilu ambaye ni mume wa marehemu, zinadai kuwa kabla ya tukio hilo, Rehema na mumewe walikuwa kwenye ugomvi mzito usiokuwa na dalili ya kumalizika.
MAELEZO YA UPANDE WA MWANAUME
Habari zinadai kwamba marehemu alikuwa akidaiwa fedha na mfanyabiashara mmoja (hakutajwa jina) lakini mumewe hakulijua deni hilo mpaka siku za mwisho za uhai wa Rehema ambapo hata hivyo hakumuuliza.
Aidha, ikadaiwa kwamba mfanyabiashara huyo alikuwa akimdai marehemu kwa vitisho kwamba asipolipa atamwambia mumewe, jambo ambalo mwanamke huyo hakutaka litokee.
Siku ya tukio, habari zinadai kuwa marehemu aliamka mapema na kufanya shughuli za nyumbani na baada ya muda inadaiwa alikunywa sumu ambayo haikujulikana ni ya aina gani.
Ikazidi kudaiwa kuwa baada ya kitendo hicho, mumewe alifanya juhudi za kumnywesha maziwa ili kuokoa uhai wake lakini ilishindikana kufuatia mke kumzidi nguvu mumewe na kukimbilia kwenye gari na kuondoka nyumbani kwenda kusikojulikana.
“Mwanamke alipokunywa sumu, mumewe (Simon)alifanya juhudi za kumpa maziwa ili kuokoa maisha yake lakini alizidiwa nguvu, mke akatoka na gari na kwenda kusikojulikana.
“Simon alikwenda kukutana na mdai wa mkewe na kumlipa fedha zake akiamini mkewe alikunywa sumu kwa sababu ya deni, baada ya malipo akampigia simu mkewe ili kumtaarifu lakini simu hiyo ilikuwa inaita na kukatika, baadaye haikupatikana kabisa,” alisema ndugu huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake gazetini.
Kuanzia hapo, ndugu walianza kumsaka Rehema mpaka Agosti 2 mwaka huu habari zilipopatikana habari kwamba kuna gari limekutwa limeteketea kwa moto kwenye msitu wa Mabwepande. Mtu aliyedaiwa ndiye alikuwa dereva naye alikuwa ameungua na kubaki majivu na fuvu likiwa sehemu ya kiti.
Hata hivyo, ndugu hawakutaka kuweka msiba wakiamini aliyefariki dunia kwa moto huo anaweza asiwe Rehema. Ili kujiridhisha na hilo, walichukua mabaki hayo na kuyapeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa vipimo vya DNA.
MUME ANA SIRI NZITO?
Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo zinadai kuwa huenda Simon ana siri nzito juu ya kifo cha mkewe Rehema kwani haingii akilini mume kuzidiwa nguvu na mkewe wakati wa kumsaidia kumnywesha maziwa.
Aidha, mpenyesha habari huyo aliendelea kufunguka kwamba ilikuwa ni kawaida kwa wanandoa hao kutibuana na mke kwenda anakojua hata kwa siku tatu bila mwanaume kujishughulisha kumtafuta.
MAELEZO UPANDE WA MKE
Agosti 6, 2012 mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa marehemu Rehema, Mbezi Beach, Dar na kukuta watu wachache ikidaiwa hali hiyo ilitokana na wengi kutoamini kama Rehema alifariki dunia. Mume wa marehemu hakuwepo msibani hapo bila kujulikana alikokwenda.
Alipotafutwa ndugu wa marehemu kuzungumzia suala hilo, kila mmoja aliruka na kudai mwenye uwezo wa kuzungumzia jambo hilo ni mama mzazi ambaye naye aligoma kusema lolote.
“Mwenye uwezo wa kuzungumzia suala hilo ni mama mzazi lakini amegoma kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa vile anahisi kuna mchezo mchafu umefanyika,” alisema ndugu mmoja.
Hata hivyo, mtu mmoja wa karibu na familia ya marehemu alisema kuwa habari kamili juu ya msiba huo zitapatikana mara baada ya kupata vipimo kutoka kwa mkemia mkuu kubaini kama kweli aliyekutwa ameteketea kwa moto ndani ya gari ni Rehema.
“Ni vigumu kulizungumzia suala hili kwani linatatanisha, unaweza kusema aliyekufa ni Rehema na matokeo ya mkemia mkuu yakitoka yakaonesha tofauti, inaweza kuleta shida, tusubiri majibu kwanza,” alisema mtu huyo bila kutaja jina lake.
MAJIBU YA MKEMIA MKUU YATOKA
Agosti 10, 2012 mmoja wa ndugu wa marehemu alimpigia simu mwanahabari wetu na kumweleza kuwa majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali yametoka na kubaini kwamba aliyekufa ni Rehema Nungu.
“Kama unavyosikia vilio hivyo, nipo msibani, majibu ya mkemia mkuu yamebaini aliyekufa ni Rehema Nungu, taratibu za mazishi zinafanywa sasa ila naomba muende nyumbani kwa Simon mtapata habari kamili,” alisema ndugu huyo na kusisitiza kuwa kama msiba utafanyika kwa mume wa marehemu, hawatakwenda ila watakwenda makaburini tu.
NYUMBANI KWA SIMON
Baada ya kupata taarifa hizo, waandishi wetu walifika nyumbani kwa Simon, Tegeta Nyuki, Dar na kumkuta msemaji wa familia hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Dedu.
Dedu alipopewa pole ya msiba na kutakiwa kueleza sababu za kifo cha marehemu, alisema waulizwe polisi yeye hawezi kusema chochote licha ya kukutwa na picha ya marehemu mkononi.
“Siwezi kusema chochote, kamuoneni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ana habari zote za msiba huu, naomba mniache niendelee na taratibu za hapa,” alisema Dedu.
HUYU HAPA KAMANDA WA MKOA WA PWANI
Agosti 10, 2012 mwandishi wetu alitinga katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu kwa lengo la kujua chochote kuhusu kifo cha mwanamke huyo lakini hakuwepo, ikabidi apigiwe simu yake ya kiganjani ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli majibu ya tukio hilo yametoka, mtu aliyeteketea kwa moto ndani ya gari ni Rehema lakini sipo katika nafasi nzuri ya kuongea kwani niko Muhimbili nashughulikia majeruhi wa ajali ya wanakwaya wa kutoka Kenya.
“Hata kesho (Agosti 11) sitakuwa ofisini kwani nitakuwa bado nashughulikia suala hilo, waliofariki ni raia wa nje hivyo ni vyema nikahakikisha wanasafirishwa kurudi kwao,” alisema Kamanda Mangu.
UTATA
Asubuhi ya Agosti 11, 2012, wanahabari wetu walidamkia nyumbani kwa Simon ili kutaka kujua taratibu za mazishi.
Nje ya nyumba alikuwepo Dedu na mzee mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, akasema yeye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya mazishi. Wawili hao waligoma kuongea chochote kwa madai yaleyale, suala liko polisi.
Hata hivyo, muda huohuo simu ya Dedu iliita, alipopokea ilionekana kupigwa na ndugu mmoja wa marehemu ambaye alisema mazishi ya mabaki ya mwili wa Rehema (fuvu na majivu) yangefanyika Jumamosi au Jumapili iliyopita lakini baada ya kupata kibali kutoka kwa mkemia mkuu.
Baadaye habari kutoka ndani ya familia ya Rehema zilisema kibali cha kuzika masalia ya mwili wa marehemu kilikuwa kipatikane jana Jumatatu.
Marehemu Rehema ameacha watoto wawili, Ngimba na Muheri.
Wasomi UDSM Waikosoa Bajeti Ya Elimu ‘Live’
Baadhi ya maofisa kutoka taasisi ya HakiElimu
TAASISI ya HakiElimu leo jijini Dar es Salaam imewakutanisha baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walimu pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ambapo waliishuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu ikiwasilishwa ‘live’ mjini bungeni mjini Dodoma kabla ya kutoa maoni yao.
Wadau hao wa elimu kwa pamoja waliishuhudia kupitia king’amuzi bajeti ya Wizara ta Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwasilishwa ‘live’ wakiwa kwenye mkutano kisha baadaye kutoa maoni yao jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2012/13, Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo alisema ameshangaa bajeti hiyo kutouona mgomo wa walimu wa juzi pamoja na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ni tatizo kwa elimu na kuiingiza kama changamoto.
“Binafsi kati ya vitu ambavyo vimenishangaza ni bajeti hiyo kutotaja mgomo wa walimu katika bajeti iliyopita kuwa ni miongoni mwa changamoto za wizara hiyo…na hata migomo ya vyuo vikuu,” alisema Dk. Mkumbo alipokuwa akijadili katika mkutano huo.
Alisema wizara imetaja kufanya vizuri katika elimu upande wa msingi na sekondari kwa kidato, lakini imekwepa kutoa mafanikio kwa kidato cha tano na sita eneo ambalo limefanya vibaya kwa matokeo ya hivi karibuni. Alikosoa kiwango cha uwiano kati ya wanafunzi na walimu kilichotatolewa kwa sasa (1:46) kwani idadi kubwa ya walimu wapo shule za mjini huku hali mbaya ikiwa vijijini.
Aidha aliongeza kuwa wizara pia imeshindwa kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ya mara kwa mara ni changamoto hivyo kushindwa kueleza katika bajeti yake. “…karibu asilimia 80 ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu imesababishwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, lakini hili halikutajwa katika bajeti ya waziri,” alisema msomi huyo.
Kwa upande wake Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM akizungumza katika mkutano huo alisema bajeti iliyowasilishwa ni ya kawaida hivyo ni vigumu kumaliza changamoto lukuki za elimu zinazoikabili wizara hiyo.
Alisema bajeti imejivunia ongezeko la idadi ya vyuo vikuu lakini imeshindwa kuonesha ubora wa vyuo hivyo jambo ambalo ni hatari endapo litaachwa, bila udhibiti. “…Twaweza kuwa na vyuo vingi lakini suala la ubora ni tatizo lingine. Pia uandikishaji wa idadi kubwa ya wanafunzi unatakiwa kulinganishwa na waliokusudiwa kuandikishwa…maana twaweza jivunia kiwango kinapanda kumbe tunadanganywa na ongezeko la idadi ya watu,” alisema msomi huyo.

Dk. Ulimboka Awekwa Mafichoni
WINGU limegubika sakata la kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka siku moja baada ya kurejea nchini, huku watu wake wa karibu akiwamo baba mzazi, wakigoma kusema chochote kumhusu.Dk Ulimboka alirejea nchini juzi akitokea Afrika Kusini alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kwa takriban mwezi mmoja na nusu, baada ya kutekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo na Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.
Ingawa wakati wa ugonjwa wake baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakitoa maelezo mbalimbali, jana wote waligoma kusema chochote, huku jitihada za gazeti hili kumpata nyumbani kwake zikigonga mwamba.Baba mzazi wa Dk Ulimboka, Stephen Mwaitenda aliweka wazi kuwa ni vigumu kumwona daktari huyo jana.Takriban watu wote waliofika nyumbani kwa Mzee Mwaitenda jana kumjulia hali Dk Ulimboka waliambiwa kuwa hayupo nyumbani.
Mwaitenda alilieleza gazeti hili kuwa ana furaha kuwa mtoto wake alirejea nchini salama licha ya kupelekwa Afrika Kusini akiwa taabani kutokana na kipigo.
Alipotakiwa kueleza juu ya kile kilichompata, mtoto wake huyo alisema: "Mungu na Steven mwenyewe (Dk Ulimboka) ndio wanaojua kilichotokea."Aliongeza: “Kweli nimefurahi kwamba mwanangu amerudi, lakini siwezi kuelezea nini kilimtokea alipotekwa," alisema Mwaitenda.Alisema Dk Ulimboka hayupo nyumbani na hajui kwamba angerudi wakati gani. "Hata kama angekuwapo, ni vigumu kumwona," alisema.
Kauli ya Katibu wa Madaktari

MAOFISA WATATU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WATIMULIWA KAZI
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi watatu wa wizara hiyo kutokana na ukiukaji wa sheria na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar.
Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabiri.
(1) Waliofukuzwa kazi kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:
- Bw. Obeid F. Mbangwa - Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori,
- Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,
- Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.
(2) Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:
- Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.
(3) Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:
- Bibi Martha P. Msemo - Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.
- Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.
(4) Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.
- Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.
(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:
- Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
- Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.
Wahusika wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.
Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
13 Agosti 2012
(Imetolewa kwenye Press Conference iliyofanyika Katika Viwanja vya Bunge Dodoma tarehe 13 Agosti 2012)

Subscribe to:
Posts (Atom)