Tuesday, July 2, 2013
Saturday, June 29, 2013
HATARI LAKINI SALAMA!
Randy Miller akicheza na chui wake Eden.
Chui Eden akiwa amemdondosha chini mwalimu wake Randy
Randy akiwa chini baada ya kudondoshwa na Eden.
Marafiki hao wawili wakiwa katika pozi.Taswira hapo juu zinamwonyesha Bwana Randy Miller (45) akicheza na chui wake aitwaye Eden ambaye amemfundisha
jinsi ya kufanya mashambulio yasiyo na madhara na ambaye amekuwa akimtumia katika kucheza filamu mbalimbali.

Mambo 20 ya kusisimua kuhusu Obama
RAIS wa Marekani, Barack Obama, anatarajia kutua Tanzania Jumatatu. Watanzania wengi wanamsubiri kwa hamu, lakini je wanayafahamu mambo yanayovutia kuhusu rais huyo? Makala hii inayachambua mambo 20 ya kufurahisha kuhusu Obama.
1. Asili
Obama ni mchanganyiko wa damu ya Kenya, Ireland na England.
2. Namba 44
Ni Rais wa 44 wa Marekani. Rais wa kwanza alikuwa, George Washington, ambaye alitawala kuanzia mwaka 1789 hadi 1797.
3. Anapenda TV
Obama anapenda kuangalia televisheni. Anapenda kipindi cha ‘The Wire’. ‘The Wire’ ni tamthilia inayorushwa kwenye televisheni na inahusu upelelezi wa polisi.
4. Wa Kwanza
Obama ni rais wa kwanza wa Marekani ambaye amezaliwa Hawaii.
5. Ndugu yake
Rais Obama ana dada mmoja tu, anaitwa Maya. Hata hivyo Obama na Maya wamechangia mama tu, baba ni tofauti.

SIMULIZI ZA MZEE MADIBA; MANDELA BONDIA ALIPOKUTANA NA BONDIA…!
Ndugu zangu, Kuna simulizi nyingi za Mzee wetu Madiba. Hakika, Nelson Mandela hajawahi kuwa mpenda makuu. Mzee Mandela yuko simple sana, ni tangu enzi za ujana wake. Lakini, kuna ambao hawajui kuwa Mandela anapenda sana mchezo wa ngumi, na kuwa , yeye mwenyewe aliwahi kuwa bondia.
Kuna wakati akiwa Ikulu kama Rais, Mandela alipata habari za bondia wa Afrika Kusini aliyetwaa taji la kimataifa. Mandela alifurahishwa sana na habari hizo. Akataka ampongeze mwenyewe bondia huyo.Siku moja akiwa na wasaidizi wachache sana, Mandela alikwenda hadi nyumbani kwa bondia huyo. Alihakikisha kuwa bondia huyo yuko nyumbani kwake. Alipofika, Mandela aliwaambia wasaidizi wake wakamwambie bondia huyo kuwa nje kuna mtu anayehoji ubingwa wake. Wamwambie kuwa mtu huyo ( Nelson Mandela) anadai kuwa yeye ndiye bingwa wa uzito huo katika Afrika Kusini ( Nelson Mandela!) Kwamba anataka mkutane mpange siku ya kupigana ili apatikane mshindi halali wa taji hilo.
Basi, bondia yule akapokea habari hizo na akatamani sana amwone huyo anayedai kuwa ana ubavu wa kupambana naye. Alipotoka nje akakutana na Nelson Mandela akiwa amesimama getini na amekunja ngumi yake. Akatania; “ Nimekuja kwako tuzipige ili dunia imjue bingwa halisi!”
Ikawa ni furaha kubwa kwa bondia yule. Hakuamini macho yake. Kuwa Rais wa nchi amekuja nyumbani kwake kumpongeza. Kumpongeza kwa jambo kubwa alilolifanya kwa taifa la Afrika Kusini.
Na Mandela akawa tayari kuingia nyumbani kwa bondia huyo na kunywa nae chai!
What a Great Leader Of Africa! Yes, Nelson Mandela!
Maggid Mjengwa,
Iringa.

OBAMA, MANDELA SIRI NZITO!
NDEGE YA OBAMA NI NYUMBA INAYOTEMBEA AIR Force One ni ndege kubwa ya Rais wa Marekani. Ndege hii ina sifa nyingi kama ndege nyingine, lakini ina nyongeza ambayo kwenye ndege nyingine hakuna. Air Force One ambayo imewahi kuchezewa filamu iliyoitwa kwa jina hilohilo na staa wa muvi za Hollywood, Harrison Ford imeonekana ndiyo ndege yenye usalama zaidi duniani. SIFA KUBWA: Ndani ya ndege hiyo kuna ofisi ya rais, jiko, chumba cha mikutano, bafu, sehemu ya kuvalia nguo, eneo la kufanyia mazoezi ‘gym’ na chumba cha mawasiliano. Ndiyo maana inasemwa ni nyumba inayotembea. Pia kuna chumba cha maafisa wanaomlinda rais, sehemu yao ya kufanyia mkutano wakipata dharura na zahanati kama rais akiugua ghafla wakati ndege ipo angani. Si hayo tu, kuna chumba chenye simu 85 za mezani na Tivii 19 kwa ajili ya kupata habari za kidunia wakati ndege ipo juu. Ndege hiyo haikamiliki kuiita Air Force One bila kutambulisha sehemu maalum ambayo hutumika kijeshi kumkwepesha adui anayetaka kuilenga kwa lengo la kuilipua.
AIR Force One ni ndege kubwa ya Rais wa Marekani. Ndege hii ina sifa
nyingi kama ndege nyingine, lakini ina nyongeza ambayo kwenye ndege
nyingine hakuna.
Air Force One ambayo imewahi kuchezewa filamu iliyoitwa kwa jina hilohilo na staa wa muvi za Hollywood, Harrison Ford imeonekana ndiyo ndege yenye usalama zaidi duniani.
SIFA KUBWA:
Ndani ya ndege hiyo kuna ofisi ya rais, jiko, chumba cha mikutano, bafu, sehemu ya kuvalia nguo, eneo la kufanyia mazoezi ‘gym’ na chumba cha mawasiliano. Ndiyo maana inasemwa ni nyumba inayotembea.
Pia kuna chumba cha maafisa wanaomlinda rais, sehemu yao ya kufanyia mkutano wakipata dharura na zahanati kama rais akiugua ghafla wakati ndege ipo angani.
Si hayo tu, kuna chumba chenye simu 85 za mezani na Tivii 19 kwa ajili ya kupata habari za kidunia wakati ndege ipo juu.
Ndege hiyo haikamiliki kuiita Air Force One bila kutambulisha sehemu maalum ambayo hutumika kijeshi kumkwepesha adui anayetaka kuilenga kwa lengo la kuilipua.

Friday, June 28, 2013
TASWIRA ZA MAPOKEZI YA RAIS OBAMA NCHINI SENEGAR
Pichani juu ni taswira za rais wa Marekani, Barack Obama alivyopokelewa na rais wa Senegal, Macky Sall jana jijini Dakar nchini Senegal. Rais Obama yupo ziarani barani Afrika ambapo atatembelea nchi za Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Wednesday, June 26, 2013
Mzee Mandela afanyiwa maombi maalum
ASKOFU mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria. Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana.
Chanzo: bbcswahili

Mzee Mandela bado yuko hali mahututi
RAIS mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki.Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza kuidhibiti hali yake.
Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa.Mapema leo familia yake ilimtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.
Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.
Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana.

UCHAGUZI WA ARUSHA WAAHIRISHWA TENA ILI KUIMARISHA HALI YA AMANI NA UTULIVU
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi wa madiwani kata nne za Arusha hadi Julai 14 kuruhusu kurejea utulivu baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema ulioathiri uchaguzi huo wiki iliyopita.
Bomu hilo lilirushwa Juni 15 na mtu asiyejulikana katikati ya mkutano wa Chadema katika viwanja vya Soweto, mjini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa na uchaguzi huo wa Juni 16 kulazimika kuahirishwa.
Baada ya tukio hilo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Arusha aliuahirisha hadi Juni 30, lakini jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema utafanyika Julai.
Kata zinazohusika ni Elerai, Kimandolu, Thani na Kaloleni. Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Lubuva alisema walipotangaza kuwa uchaguzi ungefanyika Juni 30 waliamini kuwa hali ya utulivu na amani ingekuwa imetengemaa.

ULINZI WA RAIS OBAMA JIJINI DAR NI BALAA....MITAMBO MBALIMBALI YA MAWASILIANO IMEFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIA
Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.
Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERA
Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.
“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.
Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.

Subscribe to:
Posts (Atom)

.jpg)

.jpg)