RAIS wa Marekani, Barack Obama, anatarajia kutua Tanzania Jumatatu. Watanzania wengi wanamsubiri kwa hamu, lakini je wanayafahamu mambo yanayovutia kuhusu rais huyo? Makala hii inayachambua mambo 20 ya kufurahisha kuhusu Obama.
1. Asili
Obama ni mchanganyiko wa damu ya Kenya, Ireland na England.
2. Namba 44
Ni Rais wa 44 wa Marekani. Rais wa kwanza alikuwa, George Washington, ambaye alitawala kuanzia mwaka 1789 hadi 1797.
3. Anapenda TV
Obama anapenda kuangalia televisheni. Anapenda kipindi cha ‘The Wire’. ‘The Wire’ ni tamthilia inayorushwa kwenye televisheni na inahusu upelelezi wa polisi.
4. Wa Kwanza
Obama ni rais wa kwanza wa Marekani ambaye amezaliwa Hawaii.
5. Ndugu yake
Rais Obama ana dada mmoja tu, anaitwa Maya. Hata hivyo Obama na Maya wamechangia mama tu, baba ni tofauti.
6. Mchezo wake
Rais Obama ni shabiki mkubwa wa baseball na timu anayoipenda ni Chicago White Sox.
7. Nguvu ya ushawishi
Katika miaka ya 2005 na 2007, Jarida la Time lilimchagua kuwa mmoja wa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani.
8. Anapenda kikapu
Licha ya kuwa mpenzi wa baseball, Obama anapenda kucheza mpira wa kikapu na poker.
10. Majina ya utani
Wakati akiwa mtoto huko Hawaii wanafunzi wenzake walikuwa wakimwita Barry. Majina mengine ya utani ya Obama ni Bama na Rock.
11. Vyuo vikuu
Vyuo vikuu alivyopitia Obama ni Chuo Kikuu cha Columbia na Chuo cha Sheria cha Harvard.
12. Avunja mwiko
Barack Obama amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika na Marekani. Wamarekani wanapenda kuchagua watu weupe.
13. Mshindi wa Grammy
Mwaka 2006, Obama alipata tuzo ya Grammy ya Matamshi Mazuri ya Kurekodiwa. Tuzo hiyo ilitokana na jinsi Obama alivyojieleza kwenye rekodi ya ‘Dreams From My Father.’
14. Mtoko wa kwanza
Rais Obama alipoanza uhusiano na mke wake, Michelle Robinson, siku ya kwanza alimtoa kwa kumpeleka kuangalia filamu ya ‘Do The Right Thing’, ilikuwa mwaka 1989.
15. Anajuta
Rais Obama amewahi kukiri kwamba wakati akiwa mdogo aliwahi kujaribu mihadarati. Lakini alisema anajuta mpaka sasa na akaongeza kuwa hayo ni makosa ya ujana.
16. Baba mzuri
Obama anapokuwa Marekani huhakikisha yupo nyumbani kila wakati wa usiku na husoma kitabu cha ‘Harry Potter’ kwa ajili ya binti yake, Malia, ili alale.
17. Imani
Obama ni Mkristo, lakini baba yake Barack Hussein Obama na mama yake Ann Dunham si wafuasi wa dini hiyo.
18. Jina Barack
Jina la kwanza la Obama, ‘Barack’ ni neno la Kiarabu likimaanisha baraka.
19. Rais Mwanasheria
Rais Obama ni Mwanasheria wa 27 kupewa urais duniani.
20. Ndugu mwigizaji
Mwigizaji nguli, Park Overall, ana undugu na Rais Obama.
No comments:
Post a Comment