Monday, November 5, 2012
Huyu ndio Miss Tanzania 2012
Mshindi wa Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred (katikati)katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester, Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa, Edda ni Miss Kigamboni na Kanda ya Temeke.
Hongera Brain
Napenda kutoa pongezi kwa kijana wangu Brain kwa kumaliza kidato cha nne katika shule ya Tengeru Boys Arusha,Hongera sana Brain na mwenyenzi mungu akutangulie. your Aunty Faustina (Mama wa aSilialive)
Bodi Ya Utalii Washuhudia Matangazo Yao Uingereza
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi
akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge
wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband wakati ujumbe wa TTB
ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa ligi kuu
ya Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku
ya jumamosi nchini Uingereza, Bodi ya utalii Tanzania inatangaza
matangazo ya utalii wa Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika
kuchezea ligi kuu ya Uingereza (Premier Liegue) kikiwemo kiwanja cha
Sunderland FC, katika picha katikati ni Edmund Hazal Mkurugenzi wa
Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo,Bw. David
Miliband pia ni mwenyekti wa klabu ya Sunderland.
Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena kushoto mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa, David Miliband pia ni mwenyekiti wa klabu ya Suderland
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya UtaliiTanzania TTB Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani na maafisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson Mkurugenzi wa Biashara na Kevin Ball Nahodha wa zamani wa timu hiyo
Ujumbe wa Bodi ya Utalii na maafisa wa taasisi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja nje ya uwanja huo kutoka kulia ni Bw. Manase kutoka Ngorongoro, Bw. Mukhtar kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki , Mkurugenzi wa Masoko TTB Devotha Mdachi, Geofrey Meena Meneja Masoko TTB na Edmond Hazal Mkurugenzi wa kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo katika viwanja vya ligi kuu Uingereza.
Picha kwa hisani ya Fullshangweblog

Thursday, November 1, 2012
Wananchi sasa kutuma maoni kuhusu Katiba Mpya kwa ‘sms’ Jumatano, Oktoba 31, 2012
Na Mwandishi Wetu
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza namba nne (04) za simu za mkononi ambazo wananchi kwa sasa wanaweza kuzitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (‘sms’) kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Kwa mujibu wa taarifa ya Tume hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo (Jumatano, Oktoba 31, 2012) namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao kwa njia ya ‘sms’ ni 0715 (Tigo) /0767 (Vodacom) / 0787 (Airtel) / 0774 (Zantel) – 08 15 08.
“Kwa kuzingatia kuwa Watanzania wengi waliopo mijini na vijijini wanamiliki simu za mkononi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaamini kuwa njia hii ni fursa nyingine muhimu kwa Watanzania kuweza kuwasilisha maoni yao kwa Tume,” imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid.
Ili kutuma maoni, Bw. Assaa amesema, mwananchi anapaswa kufungua ukurasa wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) katika simu yake na kuandika maoni yake pamoja na jina lake kamili, jinsia, mahali anapoishi, umri, elimu na kazi na kutuma kwenda kwenye namba yoyote kati ya zilizotolewa.
Kwa mujibu wa Bw. Assaa, baada ya kutumwa, maoni hayo yatakwenda kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambapo yatafanyiwa kazi pamoja na maoni yanayokusanywa kwa njia nyingine.
Uanzishwaji wa njia hii ya ujumbe mfupi wa maandishi unalenga kuwapa fursa nyingine wananchi kutoa maoni yao. Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inapokea maoni ya wananchi kupitia mikutano ya ana kwa ana; barua pepe (maoni@katiba.go.tz); njia za posta (S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar); ukurasa wa ‘facebook’ (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na tovuti (http://www.katiba.go.tz/).
Katika taarifa yake hiyo, Tume imewaomba wananchi kutumia namba hizo kutuma maoni yao binafsi kuhusu Katiba Mpya bila kushawishiwa na watu, makundi, vyama au taasisi yoyote na kufafanua kuwa Tume inatarajia kuanza kupokea maoni ya makundi, vyama na taasisi mara baada ya kumaliza kukusanya maoni binafsi ya wananchi katika awamu ya nne na ya mwisho itakayomalizika mwezi Desemba, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)