Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus
Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari madawa ya kulevya aina ya bangi
ambayo yalikuwa kwenye magunia 97 yaliyokamatwa na askari wa jeshi hilo
katika eneo la Usa river wilayani Arumeru (Picha na Rashid Nchimbi wa
Jeshi la Polisi)
Friday, February 8, 2013
HIVI NDIVYO MATUMAINI ALIVYOPOKELEWA JIJINI DAR
Matumaini (kulia) akiwa na Bi. Mwenda (wa pili kushoto) na anayefuata (kushoto) ni msanii mwenzake Kiwewe wakisubiri gari la kumpeleka hospitali.
Bi. Mwenda akiwa amembeba Matumaini mgongoni.
Thursday, February 7, 2013
Kiongozi wa Chadema alipokwenda kumjulia hali Askofu Thomas Leizer Kabla ya Kifo chake
Askofu Thomas Leizer, katika siku za mwisho za uhai wake, akiwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Selian Hospital Arusha Centre. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe. Picha hii ilipigwa Tarehe 3 Februari 2013, ambapo viongozi wa CHADEMA (Mbowe na Lema) walifika kumjulia hali, baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa
Picha kwa Hisani ya Jamiiforums.
Picha kwa Hisani ya Jamiiforums.
Taswira bungeni leo
Baadhi ya Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakielekea katika
Ukumbi wa Mkutano wa Bunge leo Dodoma. Maafisa hao wamefanya ziara
Bungeni hapo ili kuona shughuli za Bunge,
Aggrey Mwanri akijibu hoja Bungeni
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011.
(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete azindua vitambulisho vya taifa
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyesha kitufe kuashiaria kuzindua
rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya
taifa uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel
Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said Meck Sadik.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiangalia bango lenye kitambulisho cha taifa cha Rais Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua mfumo wa Usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi

WAMA yakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 700
Taaasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) imeikabidhi hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine kontena lenye urefu wa futi 40 lenye mitambo na vifaa vya huduma ya afya vya kisasa ilivyochangiwa na Shirika linayoshughulika na utoaji wa huduma za kibinadamu la Project C.U.R.E la nchini Marekani vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika viwanja vya...
Askofu Leizer wa KKT amefariki dunia
Askofu wa Kanisala KKKT Thomas Leizer enzi za uhai wake
ASKOFU wa lKanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania ( KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer amefariki dunia alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha.
Askofu Leizer amefikwa na mauti ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kumjulia hali hospitalini hapo.Taarifa zilizolifikia hivi punde zinadai kwamba Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna Daktari wala ndugu aliyekuwa tayari kusema ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.
Waziri Mkuu alifika hospitalini hapo jana saa saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiliwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa Madaktari (ICU).
Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiliwa kuzungumza na mgonjwa huyo.
Kabla ya Waziri Mkuu kufika katika hospitali hiyo na kumjulia ali taarifa zilizowahi nkutolewa na ndugu pamoja na watu wa karibu ikiwemo uongozi wa hospitali hiyo ilidai kwamba Askofu Laizer alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika katika Hospitali ya Selian kutaka kumjulia hali.

Deni la taifa; kila Mtanzania anadaiwa Sh450,000
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza matokeo ya sensa, inayokaribia watu 45 milioni, siku chache baadaye deni la taifa lilitangazwa kufikia Sh21 trilioni huku katika wastani kila mtu akidaiwa Sh467,404. Fedha hizo zinatokana na mkopo baada ya Serikali kukopa kwa ajili ya kujenga miundombinu kama barabara, bomba la gesi, mishahara ya wafanyakazi, na...
miradi mingine.
Kwa mujibu wa taasisi isiokuwa ya kiserikali ya Tanzania Coalition on Debt and Development (TCDD), serikali inadaiwa ‘mzigo wa madeni’ unaofika Sh21 trilioni.
miradi mingine.
Kwa mujibu wa taasisi isiokuwa ya kiserikali ya Tanzania Coalition on Debt and Development (TCDD), serikali inadaiwa ‘mzigo wa madeni’ unaofika Sh21 trilioni.
Wednesday, February 6, 2013
Vivutio saba barani afrika

Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambazo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kabisa kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.
Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.
Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.
Kutoka Fullshangweblog
H BABA AMZIBA MDOMO FROLA MVUNGI....."ACHANA NA SHILOLE MKE WANGU"
MSANII wa miondoko ya bongo fleva H.Baba ameamua kufunguka juu ya malumbano yaliyotokea kwa wasanii wawili wa filamu nchini Shilole na Frola Mvungi,na kuelezea hatua ambazo amezichukua kuhusu malumbano hayo
Akiongea na safu Maisha H.Baba alisema kuwa hatua ambayo ameichukua ni kumshauri mkewake mtarajiwa Flora Mvungi kuachana na malumbano na kuendelea na kazi zake kwani wanamajukumu mazito yanayowakabili

Subscribe to:
Posts (Atom)