HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia
mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu,
Amani limeinyaka.
Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha
akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama
kuigiza kwa muda mrefu.
Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.
Tuesday, April 30, 2013
TASWIRA ZA SHOW YA DIAMOND JIJINI LONDON
Pichani juu, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akifanya makamuzi ndani ya jiji la London wikiendi iliyopita. Msanii huyo bado anaendelea na ziara yake nchini England.
LEMA ASEMA HAYA BAADA YA KUACHIWA MAHAKAMANI KWA DHAMANA
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema ameachiwa huru kwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi baada ya kusota rumande kwenye kituo kikuu cha polisi kwa siku tatu kwa kosa la kuchochea vurugu chuoni uhasibu huku baada ya kutoka akiwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kumzomea mkuu wa mkoa.
Lema alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa Tatu na robo asubuhi akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kufikishwa mbele ya hakimu Devotha Msele na ndipo mwendesha mashtaka Eliang’enyi Njiro alisimama kuanza kumsomewa mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani aliyoyafanya kwenye eneo la chuo cha uhasibu njiro jijini Arusha.
Baada ya kutoka mahakamani hapo alielekea kwenye ofisi za chama hicho na kuzungumza na waandishi wa habari huku akitoa malalamiko na kuwataka wanachama na wapenzi wa chadema kumzomea mkuu wa mkoa iwe kanisani,mskitini,au kwenye sherehe mbali mbali,
“Nawatakeni kumzomea huyo mkuu wa mkoa Magessa Mulongo na kuwa nia ya kumshtaki ipo pale pale ndugu zangu Makamanda wenzangu huyu jamaa awe msikitini kanisani kote tumzome hiyo itakuwa ndiyo salamu yetu kwake”alisema Lema
Katika hali nyingine jeshi la polisi liliimarisha ulinzi tangu nje ya mahakama hadi ndani ya mahakama hiyo kiasi utulivu katika mahakama hiyo ulionekana na shughuli kuendelea bila bughaa.
Hali kwenye mitaa mbali mbali ya viunga vya jiji la Arusha ilionekana kuendelea na mishughuliko ya kila siku kama kawaida kuliko ilivyokuwa ikionekana huko mwanzo kwenye kesi zilizokuwa zikimkabili mbunge huyo kwa wakazi wa jiji hili kuacha shughuli zao na kuelekea mahakamani kufuatilia kesi ya mbunge huyo.

BAADA YA GODBLESS LEMA KUKAMATWA AKIHUSISHWA NA UCHOCHEZI WA FUJO WA WANAFUNZI WA UHASIBU ARUSHA BAADA YA MWENZAO KUUAWA KWA KUCHOMWA KISU HATIMAE GODBLESS LEMA AACHIWA HURU KWA DHAMANA YA MILIONI MOJA
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema,ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja katika mahakama kuu kanda ya Arusha.
TUNDU LISSU AHOJIWA NA RADIO TEHRAN KUHUSU SAKATA LA KUKAMATWA MBUNGE LEMA
Nchini Tanzania sakata la kukamatwa na kuwekwa mahabusu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo.
Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimelaani hatua hiyo na kulilaumu jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kukandamiza upinzani.
Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kulituhumu jeshi la polisi Arusha kwamba, limekuwa likitumikia CCM badala ya kutumikia umma.

HUU NDO UNYAMA WALIOTENDEWA WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA
Marehemu Henry katika enzi za uhai wake....
Mwanafunzi huyo Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami. Kabla Hajafika Eneo La Malazi (Hostel) alipigiwa Simu na Mwenzake amsubiri Ili Waende Wote Hostel.
Wakati anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo...Wakati wakiendelea kuzozana, rafiki yake naye alifika.....

Picha ya marehemu Henry Koga baada ya kuchomwa kisu na
kufariki hapo hapo katika chuo cha uhasibu
Arusha.....Mwanafunzi huyo Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami. Kabla Hajafika Eneo La Malazi (Hostel) alipigiwa Simu na Mwenzake amsubiri Ili Waende Wote Hostel.
Wakati anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo...Wakati wakiendelea kuzozana, rafiki yake naye alifika.....

Majibu Ya Wanafunzi Hao Hayakuwafurahisha Watu Hao Na Ndio Walipochomoa Kisu Na Kumchoma Mmoja wa Vijana Hao Tumboni Na Shingoni na Kupoteza Maisha Hapo Hapo....
Mauaji hayo yamesababisha vurugu kubwa chuoni hapo zilizopelekea kupigwa mawe mkuu wa mkoa
"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER
Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo. Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.
Source: Mwananchi

"SIONI TATIZO KWA LULU MICHAEL KUPIGA PICHA NA PENNY....HUO NI UMBEA WA MAGAZETI"..WEMA SEPETU
Hivi karibuni zilisambaa picha za Lulu Michael akiwa katika picha ya pamoja na Penny....
Picha hizo zilizua utata mkubwa miongoni mwa watu huku kundi kubwa likidai kuwa picha hizo zimepigwa makusudi kwa lengo la kumuumiza Wema Sepetu...
Lulu Michael akiwa na Penny
Madai hayo yaliandikwa kwa kina na gazeti moja la udaku hapa nchini likisimulia ugomvi uliopo kati ya Penny na Wema Sepetu.....

"SIWAOGOPI MATAIRA WANAONIPONDA....MUNGU PEKEE ANAWEZA NA SI HAO TUMBIRI".....HII NI KAULI YA DIAMOND
Watu kadhaa wamekuwa wakimponda Diamond baada ya kwenda LONDONI kwa madai kuwa ni mshamba wa jiji na limbukeni ....
Madai hayo yamekuja baada ya msanii huyu kuanza kuyashobokea magari ya kifahari kwa kupiga nayo picha na kuzirusha hewani.....
Baada ya kuona mizengwe ya watu imekuwa mingi, Diamond ameamua kuwajibu kwa kupost jumbe huu

NAWASHUKURU SANA WADAU WANGU.
Hakika nawashukuru sana wote mliokuwa nami katika kipindi hiki cha kuumwa kwangu mungu awaongezee pale mlipotoa kwa ajili yangu.Pamoja na kwamba sikuweza kutupia vitu humu lakini hamkuacha kuperuzi habari. Nawahakikishia kuanzia sasa kila kitu kitakuwa kama kawaida habari za kumwagaaa.Nawapenda sana Asanteni kwa sapoti yenu.
Monday, April 15, 2013
MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/-
Na Boniface Wambura, TFF
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458.
Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.
WATAZAMAJI 11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO
ZITTO KABWE AIKANA NAMBA YAKE YA SIMU LIVE BAADA YA CHADEMA WENZAKE KUDAI NI GAIDI NA ACHUNGUZWE
Sasa nashawishika kuamini kuwa CHADEMA wana lao juu ya mipango ya kigaidi...
Jana Mabere marando alitoa tamko refu sana lenye namba za simu kibao za watu mashuhuri akitaka mahakama ichunguze simu zao ikiwemo ya Zitto Kabwe.....
SWALI LA KUJIULIZA:
-Kwanini Mabere Marando anatoa tamko muhimu kama hili bila kuhussisha viongozi wa juu kama Zitto?
-Matamko ya nini wakati kesi iko mahakamani?
-Kwanini chadema inaendelea kulizungumzia hili swala nje ya mahakama huku wanaharakati wa chadema kama Mwanakijiji wakiwa wameshaanzisha harakati za kutaka kesi ifutwe kwa swala kuzungumziwa nje ya mahakama?
HUU NI UJUMBE WA ZITTO AKIKANUSHA KUHUSIKA NA UGAIDI
( HAPA AMEANZA KWA KUNUKUU SEHEMU YA RIPOTI YA MABERE:)

UGOMVI WA CHADEMA NA CCM WAFIKIA PABAYA......MABERE MARANDO AYAANIKANI MAWASILIANO NYETI YA VIONGOZI WA CCM
TAMKO LA CHADEMA KUHUSU NJAMA ZA KUKICHAFUA ZINAZOFANYWA NA GENGE LA VIONGOZI WAKUU WA CCM NA VYOMBO VYA DOLA, LIMETOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO, MACHI 14, 2013 NA MJUMBE WA KAMATI KUU NA MWANASHERIA WA CHAMA, MH. MABERE NYAUCHO MARANDO
Ndugu waandishi wa habari;
LEO tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.
Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.
Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.
Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa.

Subscribe to:
Posts (Atom)