Mzee Bob Makani enzi za uhai wake.
Naibu Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania na Katibu Mkuu wa kwanza wa
Chadema, ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Bob Makani, amefariki
dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.
Habari za kifo chake zimetolewa na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Chama
hicho, Freeman Mbowe, ambaye amesema kuwa, Bob Makani amefariki dunia, baada ya
kuugua kwa muda mrefu, na mwili wake umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Kufuatia kifo cha mwasisi huyo wa chama hicho, sasa Chadema wamekatisha
ziara za kuimarisha uhai wa chama zilizokuwa zikiendelea katika mikoa ya kusini
mwa Tanzania.
No comments:
Post a Comment