Nitajaribu kuandika kadri ya alivyosema. Nitamnukuu kadri ya alivyosema,
lakini ni wazi sitaweza kuaandika yote (ya muhimu) aliyoyasema na kwa
namna ile ile aliyoisema, maana nilikuwa nikitype kwa wakati ule ule
aliokuwa akizungumza. Ni moja ya hansard nzuri kuifutilia, kuipata na
kuisoma.
Of-course baada ya mchango wake bungeni pametifuka kweli kweli. Alifuata
Mwigulu Nchemba, looh! Badala ya kuzungumzia bajeti in details akaanza
kumsakama Lissu, wapinzani na bajeti yao. Akatupa hata kitabu cha bajeti
mbadala ya Kambi ya Upinzani Bungeni ilyosomwa leo na Ndugu Kabwe Zitto
Zuberi.
Jamaa kama alivyokurupuka kujibu tamko la Zitto juu ya kufilisika hazina
kama ambavyo taarifa za Benki Kuu (BoT) kwenye mtandao zilikuwa
zinaonekana kuonesha, ndivyo ilivyokuwa leo. Anatanguliza mbele sana
kujisema juu ya uchumi grade gani vile...na kuwa aliwahi kufanya kazi
BoT. Tumsaidie. Sifa za uwezo wa mtu, kitaaluma, huwa hazisemwi mdomoni.
Zinapaswa kuonekana. People have to feel it, have to ssen it...it has
to be felt, heard not to be said with merely words.
Mmoja wa wafanyakazi wenzangu hapa, dereva, ananiambia hapa kuwa jamaa
pressure ilikuwa juu kutokana na mchango wa Lissu na Bajeti Mbadala ya
Kambi ya Upinzani ilivyoichana chane ile ya serikali. He is another
completely affected with CHADEMAphobia (or CHADEMAhegemony) akimfuatia
kwa ukaribu sana Stephen Masatu Wassira.
Baada ya hapo pia alifuatia John Komba, oohpps. I have nothing to quote
from him. Angalizo kwao; wasipokuwa makini watajikuta katika hali
iliyowasibu mwaka jana wakati wa mjadala wa Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba Mpya, ambapo baada ya KUTIFULIWA kwa hoja kabambe, wakaacha
kujadili hoja mbele yao, wakaanza kumjadili mtu (Lissu), watu (CHADEMA).
Complete out of point, out of touch. Wakaliwa kwenye mahakama kubwa ya
watu, nje ya bunge.
Anyway turudi kwenye 'headline'. Ndugu Tundu Lissu alikuwa mmoja wa
wachangiaji wa mjadala wa bajeti leo bungeni. Session ya jioni hii.
Katifua. Amesema wazi wazi kuwa wakati wa bunge la bajeti ni majira
mengine kwa ajili ya masuala ya kipuuzi. Ameita it is silly season. Na
hivyo Mkutano huu wa bajeti it is another silly season kwa sababu ni
wakati wa kujadili mambo ambayo hayatekelezeki.
Wabunge wengi (ofcoz mnawajua) wanasimama wanasema wanaunga mkono bajeti
mia kwa mia kisha wakianza kuchangia wanapinga kila kitu walichosema
awali wanaunga mkono. It is another silly season.
It
is another silly season kwa sababu serikali inaleta vitu bungeni na
wabunge wanajadili na wengine wanaunga mkono wakati inajulikana wazi
kuwa vitu hivyo havitekelezwi.
Amesema kujadili vitu ambavyo havitekelezwi ni kujidanganya wenyewe,
kudanganya watoto wetu na kuidanganya nchi hii. Ni aibu kwa kwetu kwa
wabunge wote (bunge zima).
Ametolea mfano wa namna serikali ilivyoahidi katika mkutano wa bunge la
bajeti uliopita kuwa wataweka trilioni 8.6 kila mwaka kwa ajili ya
bajeti ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Anasema kwa sababu ya kuwa ni silly season, wabunge waliitwa Saint
Gasper na Rais, wakalishwa, wakanyweshwa juu ya Mpango wa Maendeleo wa
Miaka Mitano. Lakini katika bajeti ya mwaka jana mpango huo ukatengewa
trilioni 4. (something), walipohoji wakajibiwa kuwa ni mwaka wa mpito
lakini itaanza rasmi mwaka huu.
Lakini mwaka huu tena mpango huo umetengewa trilioni 4.5 badala ya
trilioni 8.6 kama ilivyoahidiwa. “They knew they were lying, we knew
they were lying, we should be ashamed to this government, ashamed to
this budget…ashamed to these Members of Parliament kwa sababu ndiyo
wanaopitisha bajeti hii…(hapa Lukuvi akaingilia juu ya matumizi ya lugha
za kuudhi kwa kutumia kanuni ya 64 kuwa inakataza matumizi ya lugha za
matumizi na Mwenyekiti Mabumba akasisitiza).
“Mara kadhaa wamekuja hapa na kuahidi kuwa wataziba mianya ya ukwepaji
kodi, watapunguza misamaha ya kodi. Lugha hizi zimekuwa za siku nyingi
sana. Viongozi wa dini wamefanya utafiti na kuja na ripoti waliyoiita
The 1 billlion Dollar Question…hii ni disaster ya CCM and nobody else.
Mwaka 1998 Kigoda waziri wa madini, sheria ya madini ya mwaka 1998.
“Mwaka 1998 katika bunge hili wakati huo Waziri wa Nishati na Madini
alikuwa Kigoda, alisema kuwa sekta ya madini itakuwa ikichangia asilimia
52 ya revenue yote inayotokana na madini. Lakini mpaka sasa tunapata on
average dola milioni 100 tena katika utafiti huu wa viongozi wa dini
wanasema asilimia 65 zinatokana na kodi za wafanyakazi.
“Na sasa tumepata miungu wapya wanaitwa wawekezaji…our new gods, the
untouchable, kila ukigusa aah wawekezaji, ukigusa aah wawekezaji…what
have they done for us? Tunaambiwa kuwa eskta ya madini ndiyo inayotoa
more foreign exchange than any other…hizo fedha hizo ziko wapi…
No comments:
Post a Comment