Chama cha walimu Tanzania CWT kimesema kimeshangazwa na kauli iliyotolewa jana bungeni na Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Kassim Majaliwa kwamba chama hicho hakina mgogoro wa kimaslahi na serikali huku akitambua kwamba hiyo ishu iko kwenye majadiliano chini ya tume ya usuluhishi.
Rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba amesema hiyo kauli ni ya upotoshaji na ni kulidanganya bunge pamoja na Watanzania na kusisitiza kwamba nchi ya kuendeshwa kwa girba sio hii, kama girba za mwaka 70 zitaendelea kutumika 2012 ni kwamba unaishi na kichwa cha zamani katika ulimwengu mpya.
Amesema ” hizi girba hazitawasaidia kuwapa walimu mshahara, hazitawasaidia waliokata tamaa kurudisha ari ya kazi… kinachotakiwa ni kutafutwa ni ukweli utakaosaidia nchi kwenda mbele”
Kuhusu ishu ya walimu kuingia rasmi kwenye mgomo rais huyo wa Chama cha Walimu amesema hatua hiyo itafikiwa kama majadiliano yanayoendelea sasa hivi kati yao na serikali yatafikia pazuri.
Amesisitiza kwamba “katika mkutano wetu hatukumaliza majadiliano kwa sababu upande wa serikali wameomba siku mpaka tarehe 20 July 2012, ndio tutarudi mezani kuzungumza kama wametuletea tunachokihitaji na kama hatutakubaliana msajili atatupatia cheti kwamba tumeshindwa kukubaliana na tutaendelea na hatua inayofuata ambayo ni kupiga kura na kuingia kwenye mgomo”
No comments:
Post a Comment