Sunday, July 29, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA JUKWAA LA UHUSIANO WA CHINA NA AFRICA KATIKA KUPUNGUZA UMASKINI.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini Dar es salaam
Wa tatu toka kushoto ni Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian, wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Mhe Steven Wassira, wa pili  kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa Sierra Leone Mhe Momodu Kargbo, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango  Mipango Dkt Philip Mpango na kulia kabisa ni Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipicha picha na ujumbe toka china unaohudhruia  Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian(kuhsoto) na  Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo rasmi na Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini Dar es Salaam.

No comments: