Dk. Steven Ulimboka amerejea leo nchini bna kutyoa shukrani za dhati kwa watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa madaktari.
Ulimboka amerejea nchini wakati jamii bado ikiwa katika kizungu mkuti cha nani hasa aliyemteka na kumpa mateso makali Dk. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini na kiu ya wananchi sasa ni kutaka kujua ukweli kupitia kwake.
Daktari huyo ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa harakati za kudai haki na maslahi ya madkatari na huduma bora Hospitalini amerejea leo jijini Dar es Salaam akitokea nchini Afrika kusini ambako alipelekwa na Madaktari wenzake tangu Juni 30 mwaka ambako alikuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana.
Dk. Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaa lilidai kuwa aliyemteka daktari huyo ni raia wa Kenya ambaye tayari wanamshikilia.
Dk. Ulimboka amewasili leo majiya ya saa 8 alasiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na SA Airways na kulakiwa kwa shangwe, hoihoi nderemo na vifijo kutoka kwa ndfugu jamaa na marafiki sambamba na madaktari wenzake na wanaharakati.
Hakika Mungu yupo! Na anatenda miujiza yake, Ulimboka inakumbukwa aliondoka nchini akiwa hajiwezi kutokana na hali yake kuwa mbaya na kubebwa katika machela lakini leo amerejea mzima wa afya na anatembea mwenyewe.
No comments:
Post a Comment