Waziri wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe
WAZIRI wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe amesema serikali itabeba jukumu la kulipa mishahara ya wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA, baada ya wafanyakazi hao kucheleweshewa mshahara yao kwa kipindi cha miezi mitatu.
Kauli hiyo imekuja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kufikisha kilio chao kwa Waziri huyo kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza kutoakana ucheleweshwaji wa mishahara yao.
Akizungumza na wafanyakazi hao, kwenye ofisi za Shirika hilo (TAZARA), jijini Dar es salaam jana, Dk Mwakyembe alisema akiwa waziri wa wizara hiyo anawaahidi hatakubali kuona wanaishi bila kulipwa mishahara huku wakifanya kazikwa juhudi.
Dk Mwakyembe alibainisha kuwa serikali imepokea kilio chao hivyo italipa sh bilioni1.3 kama mshahara wa miezi miwili kati ya miezi hiyo mitatu wanayodai kuanzia leo (jana).
Aliitaja miezihiyo itakayolipwa kuwa ni pamoja na Juni na Julai ambapo amewataka viongozi wa Shirika hilo kutoa maelezo kuwa ni kwanini hadi sasa hawajalipa mishahara wafanyakazi hao.
Akizungumzia madai ya wafanyakazi hao ya kutaka kung’olewa madarakani kwa Mkurugenzi Mkuu,Mbegusita Akashambatwa na Naibu wake, Damus Ndumbalo, alisema shirika hili ni la kimataifa linalohusisha nchi mbili hivyo maamuzi yake ni lazima ya husishe viongozi wa pande zote mbili.
Aidha, alitoa onyo kuhusu vitendo vya hujuma ikiwa ni pamoja na wizi kuwa wale wote wanaojihusisha watambuwe kuwa dawa yao iko jikoni inachemka.
Katika hatua nyingine amesema amesikitishwa sana kuona kuwa wafanyakazi wa Mradi wa Ukarabati wa Train Mijini, hadi leo hawjalipwa mishahara ya miezi miwili,fedha hizo lilikwishatengwa.
“Nilisikitika sana kumkuta yule dada Mwanamisi akiwa amevaa overrol lake huku akiunganisha vyuma tena amefunga mfungo wa Ramadhani ambapo aliniambia tunafanyakazi lakini hatujalipwa mishahara inishangaza sana nataka walipwe haraka”alisema Dk Mwakyembe.
Awali Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi shirika hilo, Ernest Kiwele, alisema wamechoshwa na tabia za viongozi hao kuwa wamekuwa chanzo cha matatizo yote yanayowakabili wafanyakazi hao.
Alisema Mkurugenzi Mkuu na Naibu wake wamekuwa wakiendesha Shirika hilo kwa kujali zaidi maslahi yao na jamaa zao hata wale waliosimamishwa kazi kwa kuwalipa mishahara.
Chanzo: www.fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment