Saturday, September 29, 2012

KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA SH. 5,000, LINE UPS ZA VIKOSI SIMBA NA PRISON

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Yanga (anae kipiga kiungo wa Rwanda Haruna Niyonzima) na Simba (anae chezea kiungo wa Tanzania Mwinyi Kazimoto) itakayochezwa Jumatatu (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.

Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11 kamili jioni.

Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.

Viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000.

Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.

SIMBA vs TANZANIA PRISONS LINE UPS
Timu za Simba na Tanzania Prisons zinapambana jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Tayari makocha wa timu zote mbili Jumanne Charles (Tanzania Prisons) na Circo Milovan (Simba) wameshataja vikosi vyao.

Simba:                                        Tanzania Prisons:
01.Juma Kaseja (c)                            18.David Abdallah
02.Nassoro Masoud                             03.Aziz Sibo
17.Amir Maftah                                05.Laurian Mpalile
15.Shomari Kapombe                            16.Lugano Mwangama (c)
24.Juma Nyoso                                 15.David Mwantika
14.Mwinyi Kazimoto                            13.Khalid Fupi
28.Amri Kiemba                                07.Misango Magai
08.Ramadhan Chombo                            12.Fred Chudu
19.Edward Christopher                         14.Elias Maguri
10.Felix Sunzu                                17.Peter Michael
16.Mrisho Ngasa                               19.John Matei

Wachezaji wa akiba;
22.Wilbert Mweta                              01.Daudi Mwasongwe
23.Paul Ngalema                               04.Jumanne Elfadhili
20.Jonas Mkude                                09.Sino Augustino
12.Salim Kinje                                22.Julius Kwaga
04.Komanbil Keita                             08.Henry Mwalugala
13.Daniel Akuffor                             11.Hamisi Ally
05.Pascal Ochieng                             23.Jeremiah Juma

Refa: Paul Soleji (Mwanza)
Mwamuzi Msaidizi 1: Jesse Erasmo (Morogoro)
Mwamuzi Msaidizi 2: Mwarabu Mumba (Morogoro)

Mwamuzi wa Akiba: Israel Nkongo (Dar es Salaam

No comments: