Wednesday, September 5, 2012

KAULI YA CHADEMA KUHUSU KIFO CHA MWANDISHI IRINGA.


                                                                    Siku ya tukio.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimemuomba rais Kikwete kuwasimamisha kazi kamishna wa upelelezi jeshi la Polisi Tanzania Paul Chagonja pamoja na kamanda wa polisi  Iringa Michael Kamuhanda kwa madai kwamba wamekua wakitoa taarifa zisizo sahihi kuhusiana na kifo cha Daudi Mwangosi mwandishi wa habari wa Iringa aliyeuwawa kwa kulipukiwa na bomu akiwa anashikiliwa na polisi.

Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chadema John Mnyika amesema makamanda hao wamekua wakitoa raarifa zinazotofautiana na ushahidi wa picha pamoja na mashahidi waliokuwepo kwenye tukio.

Namkariri akisema “uchunguzi unaopaswa kuendelea unapaswa kuhusu tu ni nani hasa alietoa maagizo kigogo wa juu wa polisi? lakini polisi ambao wamehusika na tukio wanaonekana picha zao, ni askari saba walioko eneo la tukio, jeshi la polisi limekua na kawaida ya kuwakamata raia waliopo kwenye eneo la tukio panapotokea mauaji kwamba ndio washukiwa wa kwanza, ni kwa nini askari wote hawa saba wanaonekana hapa hawajakamatwa? tunataka wakamatwe mara moja kama washukiwa wakuu wa kwanza kabisa wa mauaji, uchunguzi huru kuhusu tu ni nani alihusika vipi kati ya hawa na vigogo gani wa jeshi la Polisi na Serikali walihusika kuwapa maelekezo kufanya kitendo hicho cha mauaji”

Kwenye line nyingine Mnyika amesema chama kimebaini kuwepo kwa mipango ya baadhi ya watu kutaka kukichafulia hadhi ili kionekane ni chama chenye kusababisha vurugu na kuwataka viongozi wote wa chama hicho kuhakikisha wanakua makini na aina hiyo ya watu.

Amesisitiza kwa kusema “wanakusudia kubandikiza silaha kwa hiyo tunatoa tahadhari kwa viongozi wetu kwenye mikutano yote ya Chadema kuchukua tahadhari dhidi ya watu wasiowafahamu ambao wengine watavalishwa mpaka mavazi ya Chadema ili kutekeleza malengo hayo maovu”

No comments: