Kwa hali ya kawaida utaona ni ngumu kuamini kwamba kitu kama utamaduni
kinaweza kuwa chanzo kikubwa cha uchumi kukua katika nchi husika.
Nchi ya Rwanda imekuwa moja kati ya nchi baarani Afrika ambayo
imefanikiwa kukuza na kuendeleza utamaduni na sanaaa mbao tayari imekuwa
ikichangia kalibia asilimia 60 ya mapato ya nchini na kuwapatia ajira
vijana kwa urahisi.
Mapato haya yamekuwa yakitokana na fedha za kigeni ambazo wamekuwa
wakitoa watalii kutoka nje ambao hasa wamekuwa wakihamasika kununua vitu
vizuri vya asili ambavyo vinatengenezwa kiasilia na wasanii wa sanaa za
utamaduni nchini humo.
Mbali na kuteka soko la watalii wamekuwa na vivutio vya asili ikiwemo
vyakula na ngoma.Taasisi zinazohusika na mambo ya utalii wamekuwa
mstali wa mbele kutangaza vivutio hivyo ndani na nje ya nchi
ukilinganisha na sisi wabongo ambao tunavivutio lukuki na tumeshindwa
kunufaika navyo
Sijui idara zetu hapa Tanzania zenye dhamana ya mambo haya ya utamaduni zinafanya nini.Inafahamika sisi ni the best more than Rwanda kwa vivutio,sijui tunakwama sehemu gani ama tatizo liko wapi! tunapaswa kujifunza kutoka kwa majirani zetu??? au wao wanapaswa kujifunza kutoka kwetu hii ni kweli kabisa watanzania tumebarikiwa sana Amani yetu ni moja ya kujivunia pili sisi tunaweza vijana wawezeshwa tu hasa kwenye sekta hizi za utamaduni wanafanya vizuri sana Serekali iangalie sekta ya utamaduni kwa jicho la pili...
No comments:
Post a Comment