Wednesday, November 28, 2012

Hatimae Baba Mdogo wa Mwigizaji wa Filamu Marehemu John Maganga Aeleza Mkasa Mzima toka Alipoanza kuumwa Mpaka kifo chake

Muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie John Stephan Maganga ambaye filamu yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya, ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.
Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia naye ni mwigizaji, ameelezea mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa mpaka siku ya kifo chake jumamosi asubui ya wikiendi iliyopita.

Baba mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji John alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala.

Aidha anaendelea na kusema siku ya pili yake John alimpigia simu na kumwambia bado anaumwa na wala hajisikii vizuri, kuona hivyo, baba yake mdogo akaenda nyumbani kwake na kumkuta amelala kwenye kochi anatoka jasho sana, akamuuliza, John vipi tena?, John akamjibu, tumbo linamuuma sana, ikabidi nimpigie simu Baba yake mzazi nimwambie tumpeleke Hospital Mwananyamala.

Tulipofika pale hospitali, kutokana na maelezo ya Stephano, madaktari wakaamua wampige X Ray na Utra Sound kwa sababu alikuwa na maumivu makali sana tumboni mwake. Baada ya majibu ya vipimo kutoka, madaktari, wakasema ana matatizo kwenye utumbo hivyo wanatakiwa wamfanyie upasuaji wa haraka.

Stephano aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa maana ya mimi na baba yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine za kupumulia zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa kwenye gari la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.

Baada ya kufika Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha dharura (emergence room), na baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor ambaye tunafaamiana naye na kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi kufanyiwa upasuaji kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo walidhani kuna utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia sehemu ambayo inaonekana kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo vipimo vinaonesha ina matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye tumbo ndiyo maana anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.

Baada ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye alitueleza kwamba mtaalamu wa tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja kesho yake asubuhi na kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya kupumua na sisi turudi kesho.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa ni siku ya jumamosi nilifika Muhimbili na kuonana na yule Dokta kama tulivyokubaliana usiku wa jana yake. Nilipokutana naye akaniambia nisubiri atanijulisha kinachoendelea.

Nafikiri wakati huo ndipo mambo yaliharibika, kwa sababu yule daktari ambaye alimtaja kutokuwepo jana, alikuwa ndani anamshughulikia hivyo alikuwa anajaribu achomwe sindano ambayo ingeweza punguza makali ya sumu iliovuja toka kwenye kongosho au angewekewa drip ya maji lakini inaonekana jambo hili lilichelewa kufanyika.

Muda mchache baadae Dokta alitoka na kuniambia John hatuko nae tena, amefariki. Hicho ndicho kilichomtokea John kuelekea kifo chake.Alisema baba mdogo wa muigizaji Stephano.

No comments: