Ndugu zangu,
Mara nyingi Watanzania wamekuwa wakipigia kelele kuhusu suala la ubinafsishaji lililoanza mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwamba halikwenda sawa.
Kwamba, pamoja na shinikizo la Benki ya Dunia na IMF kutekeleza Sera ya Ubinafsishaji kwa mashirika yaliyokuwa mzigo kwa serikali, lakini viongozi wetu waliyabinafsishaji hata yale yaliyokuwa na uwezo wa kujiendesha, mengi wakajiuzia wao.
Sasa inasikitisha tunapoasikia leo kwamba, mashirika 64 kati ya yaliyobinafsishwa mpaka sasa hayafanyi kazi tena.
Tujiulize, mashirika hayo ni yetu hasa; kabla ya kubinafsishwa hali ilikuwaje; sasa yamebinafsishwa kwa akina nani; na kwa nini mpaka sasa serikali inawaangalia tu wawekezaji hao ambao wameshindwa kutekeleza masharti ya mkataba?
Ikumbukwe kwamba, mpaka yanabinafsishwa, kulikuwa na wafanyakazi, ambao walikuwa na familia zilizotegemea kazi wanazofanya kwenye mashirika hayo, na kubinafsishwa kwa mashirika maana yake kumewafanya wengi wakose kazi, wengine wamepoteza maisha kutokana na ugumu wa maisha kwani kiinua mgongo walicholipwa hakikutosha.
Tuijadili zaidi, lakini isome pia hapa...wp-content/uploads/2012/11/Janet-Mbene.jpg
Kutoka kwa: Mbega Mnyama,
No comments:
Post a Comment