Matokeo ya chaguzi za nafasi 10 za wajumbe wa NEC Tanzania Bara wa Chama cha Mapinduzi zinazoendela Dodoma yametoka ni kama ifuatavyo:
1. Stephen Wassira - 2,135
2. January Makamba – 2,093
3. Mwigulu Nchemba – 1,967
4. Martine Shigela – 1,824
5. William Lukuvi – 1,805
6. Bernard Membe – 1,455
7. Mathayo David Mathayo – 1,414
8. Jackson Msome - 1,207
9. Wilson Mukama - 1,174
10. Fenela Mukangara - 984
—
Shukurani za taarifa hii: Makongoro Nyerere (via blogu yake ya Muhunda)
—
Wakati huo huo, blogu ya CCM inaripoti kuwa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kwamba uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara na Makamu Mwenyekiti Zanzibar utafanyika kesho tarehe 13 Novemba 2012.
Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,uliofanyika leo asubuhi Kizota mjini Dodoma, Nape alizungumzia kufanikiwa kwa siku ya jana, baada kila kitu kwenda vizuri kwa mujibu wa ratiba.
Pia alizungumzia ratiba ya leo, ambapo kutakuwa na Taarifa mbali mbali za kazi za chama, Taarifa za utekelezaji za ilani ya uchaguzi (Bara na Zanzibar) itasomwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar itasomwa na na Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.
Taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pia zitasomwa leo.
Akizungumzia mabadiliko ya Katiba, alisema kumekuwa na mafanikio sana baada ya mapendekezo yote kupitwa bila kupingwa, moja ya mapendekezo ni kuwepo kwa Baraza la Ushauri la Wazee, pamoja kubariki mapendekezo wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa watoke wilayani. Baada ya uchaguzi kutakuwa na mrejesho wa mijadala na kutoa maazimio ya Mkutano Mkuu.
No comments:
Post a Comment