ATCL 2Kapteni Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya
ukaguzi wa mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina
ya Dash-8 Q300 .
Marubani wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya
ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es
Salaam leo asubuhi. Hii ni baada ya wahandisi wa shirika hilo
kukamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini
Marekani. Ndege hii aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF
ambayo ilisitisha safari zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele katika
chumba cha marubani kupata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari,
2013, muda mfupi baada ya
ATCL 3Abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)
katika uwanja wa ndege wa Kigoma, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es
Salaam.
Ithaminishe
ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida, imeanza tena safari za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22.
Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.
No comments:
Post a Comment