Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B', Vicent
Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich'
walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya
Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariat
Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo
walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili
kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
No comments:
Post a Comment