Monday, January 14, 2013

RAIS KIKWETE KATIKA UFUNGUZI WA SKULI YA MLIMANI MATEMWE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wazee wa matemwe kuitumia fursa waliyopata ya kujengewa Skuli ya kisasa katika kijiji hicho kwa kuwasimamia vijana wao kupata elimu.

Rais Kikwete ameeleza hayo katika ufunguzi wa skuli mpya ya Mlimani Matmwe ambayo ni miongoni mwa skuli 19 zilizomo kwenye mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya lazima Zanzibar (ZABEID) ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema wazazi wanapaswa kuwa karibu zaidi katika maendeleo ya elimu ya watoto wao kwa kuwapatia mahitaji yao ya lazima na hata kujinyima katika baadhi ya mambo na kuwapa ushauri wa mara kwa mara.

“Fursa waliyopata vijana wenu hivi sasa ilikosekana hapa Matemwe kwa miaka mingi kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar, hivyo mchango wenu ni muhimu katika kujenga maisha bora ya baadae ya watoto wenu”, amesema Dk. Kikwete

Amewaeleza wanafunzi wa skuli hiyo kwamba wamepata bahati hivyo wanawajibu wa kuienzi kwa kuongeza juhudi katika masomo ili wapasi vizuri na kuifanya skuli hiyo kuwa miongoni mwa skuli bora hapa Zanzibar.

“Dunia inamambo mengi lakini kwa upande wenu wanafunzi shughulikieni hili moja tu la kusoma na wekeni lengo la kufika Chuo Kikuu na mambo mengine yatafuata baadae”, alisisitiza Rais Kikwwete.

Ameahidi kufanya tena mazungumzo na Benki ya Dunia kwa lengo la kupata mkopo mwengine kukamilisha ujenzi wa Daghali na Nyumba za walimu katika skuli zote 19 zilizomo katika mradi wa ZABEID.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanziania aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi kubwa inazochukua katika kuwasogezea karibu wananchi maendeleo katika sekta mbali mbali.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia Nobuyuki Tanaka amesema Benki hiyo itaendelea kuwa mshirika wa karibu zaidi katika kuimarisha sekta ya Elimu Zanzibar.

Ameeleza kuwa Benki ya Dunia imeridhishwa na kufurahishwa na namna Zanzibar ilivyopokea na kuutekeleza mradi huo kwa uadilifu na mafanikio makubwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali maalim abdalla Mzee alimueleza Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kwamba vipaumbele vya mradi huo ni kuongeza kiwango cha wanafunzi katika ngazi ya sekondari na kuimnua kiwango cha Elimu kwa kuktoa mafunzo kwa walimu,

Skuli ya Sekondari ya Mlimani Matemwe ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.6 na imejengwa na kampuni ya China Railway Jian Chang Engneering Co.(T) LTD ya Jamhuri ya Watu wa China.

No comments: