MABINGWA wa Tanzania, Simba wameendelea kupokea kipigo nchini Oman baada ya jana kufungwa mabao 3-1 na timu ya Taifa ya Jeshi ya Oman.Kiungo wa Simba, Haruna Moshi alifunga bao la
kufutia machozi katika dakika ya 69 baada ya wenyeji Jeshi la Oman kufunga mabao yao kupitia Alabab Alnoaley (22), Yones Almushefrei (89) na Kassim Said.
Simba ilianza mchezo huo kwa kasi, lakini wenyeji walitumia vizuri udhaifu wa ngome wa mabingwa hao wa Tanzania katika kuokoa mipira ya kona kufunga mabao yao.
Kocha wa Simba Patrick Liewig alisema baada ya mechi hiyo kuwa mechi ni nzuri, lakini vijana wake wamezidiwa umakini.
“Inakera kwa sababu timu inacheza vizuri lakini mnafungwa kwa sababu ya uzembe.
“Yaani mtu anapiga kona anafunga mara mbili, ni tatizo, hata hivyo bora nimeliona hili mapema kwa ajili ya kulifanyia kazi.”
Kikosi
Simba: Juma Kaseja/Abel Dhaira, 2 Nassor Said ‘Cholo’/ Haruna Shamte, 3 Paul Ngalema/ Kigi Makassy, 4 Mussa Mudde, 5 Shomari Kapombe, 6 Jonas Mkude/ Abdallah Seseme, 7 Haruna Chanongo, 8 Mwinyi Kazimoto/ Amri Kiemba, 9 Felix Sunzu/ Abdallah Juma, 10 Mrisho Ngassa/Haruna Moshi na 11 Ramadhani Chombo.
No comments:
Post a Comment