Wednesday, March 6, 2013

MHARIRI MKUU NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AVAMIWA USIKU WA MANANE NA KUJERUHIWA VIBAYA

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kibanda alivamia majira ya saa sita usiku wa kumkia leo, akitokea kwenye majukumu yake ya kila siku. Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari, akapigwa na vitu vyenye ncha kali kichwani, ametobolewa jicho lake la kushoto pamoja na kunyofolewa kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa umbali kidogo ya nyumbani kwake.

Baada ya hapo wasamalia wema walijitokeza na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu.

Watu waliomfanyia madhara hayo, hawakuweza kuchukua kitu chochote kwenye gari ambapo kulikuwemo Laptop, simu na nyaraka zingine.

Tumesikitishwa sana na unyama huo aliofanyiwa mpiganaji Kibanda na tunaomba vyombo vya Dola vifanye jitihada za ziada kuwabaini wale waote walihusika na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.

Pole saaaana Kibanda, Mungu atakujalia upate matibabu na kupona haraka. Amin.

No comments: