WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga aina ya Moramu katika machimbo yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.
Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .
Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.
Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.
Baadhi ya miili ya marehemu imetambulika kwa majina kuwa ni Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.
Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.
No comments:
Post a Comment