Saturday, April 13, 2013

MWENYEKITI WA CHADEMA ATUPWA JELA MWAKA MMOJA KWA WIZI WA MIL. 1.2

Mwenyekiti wa chadema, mtaa wa isamilo kaskazini B wilayani nyamagana Philbert Bulinjiye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kujipatia shs milioni 1,250,000 kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo, imetolewa na hakimu Vaineth Mahizi wa mahakama hiyo, kufuatia kesi ya jinai namba 196/2012, iliyofunguliwa na Vedasto Mavubhi ambaye alimtuhumu mwenyekiti huyo kuchukua kwake kiasi hicho cha fedha, kwa ajili ya kumuuzia kiwanja.

Hakimu Mahizi katika hukumu yake, alidai ameridhika na ushahidi uliotolewa na upnade wa mlalamikaji, mashahidi pamoja na wazee wa baraza hivyo kumhukumu mwenyekiti kwenda jela.

Alisema mwenyekiti huyo pamoja na Balozi Robert Byagaye wanastahili kutumikia kifungo hicho cha mwaka mmoja jela kutokana na kutiwa hatiani.

"kitendo kilichofanywa na viongozi hawa, kuwaibia raia wanaowaongoza kiutapeli kwa kuwadanganya kuwauzia kiwanja na kisha kutafuta mtu bandia kwa madai kuwa kiwanja hicho kiko katika mtaa wanaouongoza, ni udanganyifu" Alisema hakimu na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa viongozi wengine matapeli.

No comments: