Zenani ndio huyu wa nyumba ya Mzee Mandela, hawa wengine ni wajukuu na vitukuu wa Mandela.
BBC wameandika kwamba watoto wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson
Mandela Makaziwe na Zenani Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa
wasaidizi watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki wakidai kuwa
watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo
ni za thamani ya dola milioni 1.1
Kesi hiyo inakuja wakati kuna
wasiwasi kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambae aliondoka
hospitali baada ya kutibiwa mapafu akiwa tayari kalazwa hospitali mara
nne katika kipindi cha miaka miwili.
Kumekuwa na mzozo wa chinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususani picha alizokuwa anachora akiwa jela ambapo Makaziwe na Zenani Mandela waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa Bizo ambae ni Waziri wa nyumba, Tokyo Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally Chuene, hawakuwahi kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya Harmonieux Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings kulingana na gazeti la Star.
Bizos akiwa ni wakili anayeheshimika sana na ambaye pia ni rafiki wa karibu sana wa Mzee Mandela amesema kuwa watajitetea vikali katika kesi hiyo na kwamba Watoto wa Mandela walikuwa wanataka kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa.
No comments:
Post a Comment