Monday, May 6, 2013

CLOUDS WAMJIBU LADY JAYDEE....WAMEDAI KUWA AACHE KUTAPATAPA NA BADALA YAKE AKAZE BUTI

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameamua kujibu shutuma za Lady Jaydee dhidi yake. Ruge amekitumia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, kujibu rasmi shutuma hizo.

Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee anavyoendesha harakati zake na kudai kuwa anapigana kwenye vita isiyo sahihi.

“Jaydee akaze buti, anapigana na wrong war, vita yake ameidirect tofauti na mizinga yake, bunduki zake amezielekeza kusiko. Skylight Band inamsumbua, akubaliane na ukweli kwamba Skylight ndio iliyoisababishia Nyumbani Lounge kushuka ilivyoshuka, sio Lady Jaydee kama msanii.

Vita yake na bunduki zake azielekezee Skylight Band. Hajazungumza hata mara moja kwamba ndio kitu kinachosumbua. Mimi naamini kabisa akifanya hiyo kazi, Jaydee bado ni msanii mzuri, ana nguvu, afanye kazi kubwa ya kuweza kurudisha mapambano yake kisanii, kufanya kazi na aangalie tatizo lililotokea Nyumbani Lounge labda anaweza akatatua matatizo lakini sio kushambulia watu kwenye mitandao,” amesema Ruge.

Hata hivyo amesema yupo tayari kukaa meza moja na Lady Jaydee kuzungumza na kumaliza tofauti zao.


“Mimi niko tayari, kesho, kesho kutwa, kama yupo tayari na ana watu wengine wengi tu ambao wanahisi kuna matatizo binafsi ya kuongea na Clouds, twende sehemu nyingine neutral tu, tukodishe, tukae pale tusikie matatizo.

Haisaidii muziki wetu kuonekana Bongo Flava ni watu ambao kutwa ni kulalamika, kutwa ni maneno na matusi tu pale panapokuwa na matatizo.”


Ameongeza kuwa suala la wasanii wa Bongo Flava kupenda kutukana limewafanya hata wasambaji wa muziki nchini kuacha kufanya kazi nao.


“GMC kampuni iliyowapa pesa nyingi wasanii kwenye biashara sio kuwapa tu kwa kuwagawia, kwa kufanya nao biashara, sasa hivi huu ni mwaka wao wa pili na nusu hawajatoa hata albam moja ya Bongo Flava.


Wasanii wa Bongo Flava wanafikiria kwa Mamu pamefungwa lakini Mamu anaendelea na wasanii wa Gospel na wanauza vile vile.


Ruge amewaasa wasanii wa Tanzania akiwemo Lady Jaydee kuzitumia vizuri fursa za kiuchumi zinazojitokeza na sio kupenda kulalamika.


“Turudi kwenye mstari wa kuziona opportunities, turudi kwenye mstari wa kusema kwamba leo tunataka kumzungumzia Jaydee akiwa na perfume, akiwa na lipstick kama jana iliyozinduliwa na Rihanna ambayo nikaambiwa kwamba stock ya lipstick mpya ya Rihanna iliyozinduliwa ilikwisha baada ya masaa matatu.


That’s how bigger brand is supposed to be, and that’s how powerful a brand is supposed to be katika namna ya kuunganisha na fursa zilizopo. Unapokuwa na jina tumia fursa, tumia opportunities zinazokuijia wewe kujiendeleza na kujikuza.

Lakini suala la kulaumiana halitatukuza kwasababu sisi ni radio binafsi, tutafanya kile tunachokifanya sisi kwa matakwa ya wasikilizaji wetu wengi zaidi, tukiiangalia faida kama motivation, tukiiangalia social responsibility kama motivation yetu ya pili, in the long run kuangalia tunakotaka kwenda kufikia strategy ambayo kampuni yetu inajiwekea.”


Ruge pia amewakumbusha wasanii kutojisahau kwakuwa hakuna msanii anayeweza kuhit maisha yake yote.


“Tuwaandae wasijisahau, na katika hili simzungumzii Jaydee peke yake, nazungumzia wasanii wote wa Tanzania nawazungumzia kuelewa kwamba tunajisahau sana.

Tunapata hela nyingi sana, sitashangaa miaka mitatu baada ya leo, Ommy Dimpoz naye ukamsikia anaandika hivi hivi, au Diamond naye ni kwasababu hakujipanga tu.”


Kuhusu shutuma kuwa Clouds FM inaua muziki wa Bongo Flava, Ruge amesema, “inanishangaza kidogo kwasababu Clouds inategemea matangazo ya biashara kwa asilimia 95, ndio biashara yake hiyo.


 Lakini inategemea muziki wa Bongo Flava kama maudhui ya kipindi, inaanzaje kuuua, inategema wasanii wa Bongo Flava kama wasanii wa kwenda kufanya shows mkoani.”

Kuhusu msimamo wa kampuni Ruge amesema:
Msimamo wa kampuni ni kwamba tunaamini kabisa mwanadada kinara wa muziki wa Tanzania naamini atakaa na kutafakari la kufanya.

 Tunamtakia kila lakheri kwenye show yake ya tarehe 31 afanye vizuri lakini atakapokuwa tayari sisi tuko tayari kuendelea kufanya kazi, anajua cha kufanya.

No comments: