Mwandishi wetu aliyepo Mtwara ametueleza kuwa hivi sasa baadhi ya
wananchi wa eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali
ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za
kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo
asubuhi katika eneo hilo..
Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari
magereza . Mwanafunzi wa CHUNO amefikishwa hospitali Ligula na majeraha
ya risasi mguuni.
Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.
Anaelezwa kuwa katika baadhi ya mitaa hali imetulia na ni idadi ndogo ya
wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea mitaani isipokua eneo la
magomeni ambako mbomu yanaendelea kusikika huku huduma za kijamii katika
mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo usafiri, huduma za kibenki na shule
No comments:
Post a Comment