Thursday, May 16, 2013

Wadau wa utalii wakutana arusha

Wadau wa utalii kutoka halmashauri ya Wilaya ya Longido wamekutana leo hii katika mkutano wa Siku Mbili wenye lengo kuu la kuthamini na kutambua mchango wa Rasilamali zinazo wazunguka wafugaji wa halimashauri hiyo katika kujiletea uchumi kwa njia nyingine tofauti na ile iliyozoeleka.

Mkutano huo wa Wadau hao wa Utalii kutokandani ya Halimashauri ya Wilaya ya Longido ambao ulifunguliwa na Afisa wa Mazingira ya Ikolojia kutoka

mamlaka ya Hifadhi za Taifa Bwana  Alibert Mziray ambapo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kujua jinsi ya kutumia Rasilimali zilizopo hasa hasa kwa Wafugaji hao wa Loliondo.

Amesema kuwa jamii hizo zinatakiwa kutambua kuwa kina umuhimu mkubwa sana wa kutambua kuwa mazingira ya asili yaliyoazunguka wafugaji wa kiasili yana umuhimu mkubwa na ushirikiano nao hivyo inabidi wangalie jisni gani watashirikiana na mazingira yao katika maisha yao ya kila siku.

pamoja na hayo mkutano huo uliwakuatanisha wadau hao wa utalii unatarajia kujadili na kupata njia muafaka za kumsaidia mfugaji wa kiasili katika kufanya ufugajiwake uwe na tija ya kiuchumi sambamba na kuwafanya wafugaji hao kutotegemea mifugo na kuangalia njia nyingine za kiuchumi zitakazo wafanya wapate maendeleo.

Kwa sasa hivi mradi wa BFFS wilayani longido umefanikiwa kuwafikia zaidi ya wamasai 300 ambapo zaidi ya asiliamia 90 ni wanawke ambapo wamefanikiwa kwa awmu ya kwanza kuwapatia mkopo wa zaidi ya milioni 90 kwa vikundi zaidi ya 30 ambapo wamelenga kwa awamu ya pili kuvipatia vikundi vipatavyo 48 mkopo wa kuwasaidi kaya hizo za wafugaji.

Na  Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha

No comments: