WATUHUMIWA 60 wa vurugu kati ya machinga na polisi mjini Iringa akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa wanafanyiwa utaratibu wa dhamana baada ya mahakama kukubali kupewa dhamana.
Awali watuhumiwa walisomewa mashitaka matatu huku mbunge akisomewa shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu.
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na kwa sasa utaratibu wa dhamana unafanyika mbele ya mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa, Mheshimiwa Godfrey Isaya.
Mashitaka waliyosomewa watuhumiwa ni pamoja na shitaka la kwanza la mbunge ambalo ni kushawishi kufanya vurugu, huku wengine wote makosa yao yakiwa ni kufanya mkutano bila kibali, kuharibu mali kinyume na sheria ni kufanya vurugu.
No comments:
Post a Comment