Kadinali Pengo
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la
tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo
nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza
kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na
sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa
limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:
“Lengo
la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe
kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza
mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,”
alisema Pengo.
Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli
ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na
ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote
ile.
“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta
amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini
wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba
Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile.
Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa
nani,” alisema Pengo.
Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.
“Naomba
kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa
letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika
atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo,” alisema.
KADINAL PENGO ASISITIZA TENA KUWA ALIYERUSHA BOMU SI MUISLAMU.......KIKWETE AWATAKA WATU WAENDELEE KUSALI
NUKUU YA RIPOTI YA JANA
---------------------
Juzi nilibahatika kuisikiliza vyema taarifa fupi (KUNTU) iliyotolewa na mlezi wetu mkuu wa kiroho KARDINALI) ya kuujulisha umma ni nini kilichotokea kupitia chombo chake cha habari TUMAINI. Tunashukuru kwa taarifa yake hiyo ambayo kwa jinsi ilivyotolewa, nina hakika ilifanyiwa kazi ya kina kabla ya kuletwa hadharani.
Tunashawishika kuamini hivyo kutokana na jinsi kiongozi huyu wa kiroho ambavyo ameweza kutoa ripoti yake ya kiintrijensia ndani ya chini ya masaa 24! Amesema suala hili lisihusishwe kwa aina yoyote ile na dini au itikadi ya uislamu
Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
Kauli ya Kikwete
Akizungumza Arusha jana, Rais Kikwete amewataka waumini wa dini zote waendelee kusali akiahidi kwamba Serikali itaimarisha ulinzi. Alisema amekerwa na kukasirishwa na tukio hilo
.
Rais Kikwete alitanguliwa kufika Arusha na Makamu Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd ambao pia walitembelea Kanisa lililolipuliwa na baadaye kwenda kuwatembelea wafiwa na kuwafariji majeruhi hospitali.
Viongozi wote hao walitoa wito kwa Watanzania kulinda amani iliyopo na kuacha malumbano ambayo hayana tija kwa maslahi ya taifa.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment