Tuesday, January 8, 2013

EDWARD LOWASSA AVIPIGA JEKI VIKUNDI SABA VYA VIKOBA MONDULI MJINI

 Mh. Lowassa akikabidhiwa zawadi na mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu, Dawson Kaaya
wakati viongozi wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli.
 Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala mbele ya Mh. Lowassa.
 Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa (hayupo pichani).
Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na Bi Arafa Ismail kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao walikwenda kumtembelea nyumbani kwake. Kushoto kwa Mhe ni Bw. Dawson Kaaya ambaye ni Mwenyekiti wa Vikoba Monduli Mjini.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa amevipatia vukundi saba vya Vikoba vilivyopo Wilayani Monduli, kiasi cha shilingi milioni nane kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao. Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua Mtanzania kutoka katika umasikini. Kila kikundi kimepata shilingi millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi milioni moja zaidi.

SANII WA MNANDA OMAR OMAR AFARIKI DUNIA

MSANII  nyota wa miondoko ya Mnanda 'Mchiriku', Omar Omar, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Habari zilizotufikia ni kwamba, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa kutoka Hospitali ya Temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amen!

LIONEL MESSI ATWAA TUZO YA BALLON D'OR

                            Lionel Messi akiwa na tuzo yake ya Ballon d'Or.
                       Fabio Cannavaro, akionyesha jina la mshindi wa Ballon d'Or, Lionel Messi.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa nne mfululizo.
Messi (25) alifunga jumla ya mabao 91 mwaka jana na aliwashinda wachezaji wengine Andres Iniesta wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real Madrid.

Messi alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya the Ballon d'Or, tuzo ambayo hukabidhiwa mchezaji bora wa mwaka katika sherehe iliyofanyika mjini Zurich.
Mesi sasa ni mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo ya Ballons d'Or kwa miaka minne mfululizo na kuvunja rekodi ya aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa na rais wa UEFA kwa sasa, Michel Platini, ambaye alitwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo mwaka 1983, 1984 na 1985.

Hapa chini ni orodha ya kikosi cha wachezaji bora wa mwaka 2012
•Iker Casillas (Real Madrid)
•Dani Alves (Barcelona)
•Gerard Pique (Barcelona)
•Sergio Ramos (Real Madrid)
•Marcelo Vieira (Real Madrid)
•Andres Iniesta (Barcelona)
•Xabi Alonso (Real Madrid)
•Xavi Hernández (Barcelona)
•Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
•Radamel Falcao (Atletico Madrid)
•Lionel Messi (Barcelona)


WASTARA; MKE MWEMA ALIYEPIGANIA ROHO YA MUMEWE HADI DAKIKA ZA MWISHO

     Siku ambayo wapendanao hao walifunga ndoa  lakini wastara akawa na kilio cha kupoteza mguu


                                         Siku ambayo walisimamia harusi ya msanii mwenzao
SAFU ya Kali Wiki hii inakuja na tukio lililotikisa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo tasnia ya filamu kwa mara nyingine ilimpoteza muigizaji wake maarufu, Juma Kilowoko almaarufu kama Sajuki.

Kifo cha Sajuki ni pigo katika tasnia hiyo lakini zaidi kwa mkewe, Wastara Juma ambaye alifanya kila juhudi kupigania uhai wa mumewe hadi dakika za mwisho lakini Mungu akampenda zaidi na kumchukua Januari 2, mwaka huu akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa kwa matibabu.
Hatuwezi kusema mengi sana kuhusu kifo hicho kwani mnajimu maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya Hussein aliwahi kusema kwamba kupinga kifo ni kumkufuru Mungu kwa sababu hiyo ni amri yake.

Lakini ukweli unabaki palepale kwamba Sajuki na Wastara walikuwa ni wanandoa waliopendana sana katika maisha ya ndoa yao ambayo ni mafupi sana kwani walioona Juni 6, 2009 na baada ya hapo mikosi kedekede ikawa inawaandama.
Mateso ndani ya ndoa yao yalikuwa kama ni kupokezana kijiti na kuwafanya kutokwa na machozi ya huzuni. Sajuki ameugua kwa muda mrefu maradhi ya uvimbe tumboni ndiyo chanzo cha matatizo yake yote.

Katika maisha yao ya ndoa, wawili hao wamekuwa wakipokezana mateso huku likiibuka jipya la kuwatoa machozi mara kwa mara na sasa Sajuki ndiye anayewaliza watu kufuatia kusumbuliwa na maradhi ya uvimbe tumboni.

Leo tuwape historia fupi ya maisha yao ya mashaka na huzuni tukianzia Machi 12, 2009 wakati huo wakiwa wachumba tu,  Wastara na Sajuki walipata ajali mbaya ya pikipiki maeneo ya karibu wanapoishi, Tabata, Dar es Salaam ambapo mwanadada huyo alikatika mguu, hapo ndipo huzuni ya wapendanao hao ilipoanza kuwafuata. Walisikitishwa sana na tukio hilo baya katika maisha yao.
Wapendanao hao walifunga ndoa  lakini Wastara akawa na kilio cha kupoteza mguu na kutaka wa bandia ambao ulikuwa na gharama kubwa. Mungu si Athmani kwani walifanikiwa kupata shilingi milioni 7 zilizomfanya mwana mama huyo kwenda Nairobi Kenya na kupata

Historia ya maisha yao inaonesha kuwa Agosti 29, mwaka juzi Wastara alikimbizwa hospitalini na kulazwa kutokana na maradhi ya nimonia ambayo yalimjia ghafla. Lakini uchunguzi ulipofanywa alionekana pia kuwa alikuwa mjamzito, japokuwa mwenyewe alifanya siri.

Habari kwamba Sajuki ni mgonjwa zilivuma Oktoba 29, mwaka 2011 na ikagundulika kuwa alikuwa na uvimbe tumboni na saratani ya ngozi. Baya zaidi gharama za tiba zilikuwa kubwa kwani zilikuwa zikihitajika shilingi milioni sita, na wao kwa kuwa walikuwa hawana, furaha ya maisha ikadidimia
Lakini Mungu naye ana mambo yake kwani Machi 7, mwaka jana wakati fedha za matibabu India zikiwa zimepatikana kwa michango mbalimbal ndoa yao ilipata Baraka za Mungu kwa kupata mtoto. Ni bahati mbaya kwamba furaha yao haikukamilika kutokana na Sajuki kuugua.

Sajuki alifanikiwa kwenda India kutibiwa na Aprili 2, 2012 akarejea nchini kutoka katika Hospitali ya Apollo alikopelekwa kupata matibabu ambapo alisema alikuwa amepata nafuu kidogo kabla ya hivi karibuni hali kuwa mbaya zaidi na kuibua vilio upya kutoka kwa marafiki zake na hasa mkewe Wastara.
Zilisambazwa habari kwa Watanzania kuombwa kumchangia ili arudishwe India kwa matibabu lakini kabla ya mipango hiyo kukamilika Mungu akamchukua alfajiri ya Januari 2, mwaka huu na akazikwa Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mazishi ambayo yaliongozwa na Rais Jakaya Kiwete. Hakika Wastara alipigania roho ya mumewe kwa nguvu zake zote na ameonyesha upendo wa hali ya juu, anafaa kuigwa na wanandoa wengine!


Jackson makala hajafukuzwa bavicha wala chadema

 KAMANDA mpambanaji wa Chadema kutokea Babati Jackson Wilson Makala (pichani juu), amekanusha vikali habari zilizosambaa kwa watu tofauti waliokaribu nae zikimhusisha na sekeseke la kuwavua uanachama wa Baraza la Vijana Chadema ambalo limeleta sintofahamu dhidi yake baada ya  gazeti moja la kila siku kumuandika jana kuwa nae ni miongoni mwa vijana waliosimamishwa kwa muda katika baraza hilo (BAVICHA kwa makosa tofauti ya utovu wa nidhamu.

Katika mawasiliano yake na Blog hii, jioni ya leo Makala ameeleza kusikitishwa na upotoshwaji huo ambao anadai kwa kiasi fulani umemuathiri kwa kuzingatia uaminifu ambao amejijengea miongoni mwa viongozi na wanachama wengine wa chama chake, na watanzania kwa ujumla.

“Napenda kutoa maelezo mafupi kuhusu habari iliyoandikwa na gazeti la jana (jina linahifadhiwa). Mimi Jackson Wilson Makala sijasimamishwa uanachama na Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) kama ilivyotaarifiwa na gazeti hilo. Nimewasiliana na Mhariri wa habari wa gazeti… na amekiri kuwa walifanya makosa makubwa katika habari ile.

Ukweli ni kwamba Baraza la vijana CHADEMA taifa jana mchana limetoa tamko la ufafanuzi kuhusu maamuzi ya Kamati Tendaji ya BAVICHA na hakuna popote lilipotaja jina la Jackson Wilson Makala kuwa amesimamishwa uanachama.

NAPENDA KUKANUSHA KUWA HABARI ZILE NI ZA UONGO NA HAZINA UKWELI WOWOTE!
CHADEMA IS MY LIFE STYLE!” anamaliza kutoa ufafanuzi wake.

Sehemu ya habari hiyo iliyoleta utata kwa kumtaja Bw Makala kimakosa kuwa miongoni mwa vijana waliosimamishwa Chadema ilisomeka hivi ikirejea kikao cha Kamati Tendaji iliyoketi Januari 5, 2013 “Kikao hicho pia kilichukua uamuzi mgumu wa kuwasimamisha uanachama kwa muda wa mwaka mmoja, Gwakisa Mwakisando (Mbeya), Wilson Makala (Babati) na Joseph Kasambala (Mbeya)”

TAARIFA RASMI YA BAVICHA

Magazeti ya Leo Jumanne 8th January 2013







Monday, January 7, 2013

RAIS AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA WAKFU ASKOFU DKT ALEX SEIF MKUMBO WA KKKT DAYOSISI YA KATI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa na  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi  hiyo huku  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia  katika sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Wasaidizi wa Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013

PICHA NA IKULU

RAIS JAKAYA KIKWETE AANZA ZIARA YA SIKU NNE KATIKA MKOA WA TABORA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipkea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili mkoani humo jana kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Tabora  Mhe Fatma Mwassa wakati alipokuwa akisoma ripoti hiyo mbele ya Rais mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.

(PICHA NA IKULU)

MIRAJI MRISHO KIKWETE ATEULIWA KUWA “MAKAMU WA RAIS” WA IBF/AFRIKA MAENDELEO YA VIJANA

+Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa) limemteua bwana Miraji Mrisho Kikwete kuwa Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Uteuzi wa Miraji unaanza January mwaka mpya 2013.

 Katika kumteua Miraji, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Miraji ana uwezo wa kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo.

 Aliendelea kusema kuwa Miraji atakuwa anawahamashisha vijana, kuwaunganisha, kuwajengea uwezo wa kimaendeleo yatakayoratibiwa na IBF.

 Aidha, Rais huyo alisema kuwa Miraji atakuwa anabuni njia mbalimbali za kuwaunganisha vijana wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ili waweze kufaidika na miradi ya IBF ambayo inalenga kwenye elimu, kujenga vipaji pamoja na kuwaunganisha kwenye biashara ya utalii wa michezo.

 Katika mkutano wake wa mwaka uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii, nchini Marekani hivi karibuni IBF iliupokea mradi wa “Utalii wa Michezo” uliobuniwa na kuwakilisshwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtazania Onesmo Ngowi.

 Lengo kuu la mradi huu ni kulifanya bara la Afrika hususan Tanzania kuwa kitovu kikuu cha “Utalii Michezo” hivyo kujenga uchumi imara. Nchi za Tanzania na Ghana ziliteuliwa kuwa nchi za mfano kwenye mradi huu.

 Katika mradi huu, IBF itatumia mtandao walionao katika nchi zaidi ya 203 duniani kuhamasisha wanachama wake na famlia zao, wapenzi pamoja na marafiki zao kuja Afrika/Tanzania kutalii pamoja na kuwekeza katika miradi mbalimbali.

 Uteuzi wa Miraji utasaidia kuwaunganisha vijana ili waweze kuchangia na kufaidika na biashara ya utalii kwenye mradi huu umefanywa wakati muafaka.

 Miraji ambaye ni Mjasiliamali amejipambanua katika maendeleo ya jamii na ana mchango mkubwa sana katima kuendeleza vijana nchini Tanzania.

 Rais Ngowi alimwelezea Miraji kama tegemeo ambalo vijana wanalihitaji kwani wanahitaji uhamasishaji wa hali ya juu na Miraji ana uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani alishawahi kuifanya kwa kipindi kitefu.

 Miraji Mrisho Kikwete ni msomi wa chuo kikuu cha nchini Oman ambako amesomea elimu ya utawala wa biashara ambayo ndiyo lengo kuu la uteuzi wake. Ana haiba ya kupendwa na vijana pamoja na uwezo wa kujichanganya nao.

Magazeti ya Leo Jumatatu 7th January 2013





Sunday, January 6, 2013

Hoteli bora duniani ipo Tanzania.Unajua hilo

                                             Singita Grumeti Reserves

Kwa mwaka wa pili mfululizo, hoteli bora duniani ipo Tanzania.

Aidha, kati ya hoteli bora duniani 20, Tanzania ina tatu kwa jumla ikiwemo hiyo ya 1, 9 na ya 15.

Kenya wana moja tu kwenye nafasi ya 20 na Afrika Kusini ina nne, nafasi ya 7, 10, 13, na 14.

Baada ya hoteli hizi, kuna moja tu ya Afrika huko Botswana kwenye nafasi ya 17.

Bofya hapa http://www.travelandleisure.com/worldsbest/2012/hotels
kuziona zote 100 lakini kwa chini hapo kuna orodha ya 20 za kwanza.....................


Top 100 Hotels Overall

Rank '11 Name Score
1 1 Singita Grumeti Reserves, Serengeti National Park, Tanzania T+L Find 98.25
2 6 Triple Creek Ranch, Darby, Montana 98.22
3 - Southern Ocean Lodge, Kangaroo Island, Australia Debut T+L Find 97.87
4 5 Oberoi Udaivilas, Udaipur, India 97.50
5 55 Discovery Shores, Boracay, Phillippines 96.77
6 - Nayara Hotel, Spa & Gardens, La Fortuna-Arenal, Costa Rica Debut 96.36
7 39 Singita Kruger National Park, South Africa 96.33
8 19 Palacio Duhau, Park Hyatt, Buenos Aires T+L Find 96.12
9 - Ngorongoro Sopa Lodge, Tanzania 95.85
10 2 Singita Sabi Sand, Kruger National Park Area, South Africa 95.74
11 40 The Peninsula, Bangkok Hall of Fame 95.72
12 - Wentworth Mansion, Charleston, South Carolina 95.47
13 - Sabi Sabi Private Game Reserve Lodges, Kruger National Park Area, South Africa 95.40
14 - One&Only, Cape Town T+L Find 95.33
15 9 Kirawira Luxury Tented Camp, Serengeti National Park, Tanzania 95.27
16 11 The Lodge at Kauri Cliffs, North Island, New Zealand 95.25
17 20 Mombo Camp and Little Mombo Camp, Moremi Game Reserve, Botswana 95.17
18 23 Mandarin Oriental, Bangkok Hall of Fame 95.04
19 - Tu Tu'tun Lodge, Gold Beach, Oregon 95.00
20 67 Fairmont Mara Safari Club, Masai Mara, Kenya 94.84



Hata hivyo, nchi yetu inazungukwa mara kumi hadi kumi na moja na jirani zetu Kenya kwenye pato la utalii na pia hoteli za Kenya ziliopo pwani tu, zinazidi kwa idadi jumla ya hoteli zote zilizopo Tanzania Bara.