Friday, March 15, 2013

BENARD MEMBE AGEUKA MBOGO BAADA YA KUHUSISHWA NA UTEKAJI WA ABSALOM KIBANDA

 Ifuatayo ni kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe kuhusu kilichoandikwa na gazeti la Mtanzania march 13 2013 toleo namba 7255.
 “SAKATA LA KUTESWA KWA KIBANDA: Membe atajwa” na kwamba eti mimi ninahusika na vitendo vya kikatili na unyama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari, Bw. Absalom Kibanda”

“Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na habari hizo na ningependa kuwahakikishia Watanzania wenzangu kwamba sijahusika, sihusiki na sina sababu ya kuhusika kwa namna yoyote ile. Sina nia, genge wala fedha za kufanya shughuli kama hiyo.

 Katika maisha yangu yote, sijawahi kugombana naye na hajawahi kunifanyia ubaya wowote. Kwa kifupi, sina uhasama na Bw. Absalom KIbanda”
.

"VIDEO YA LWAKATARE NI FEKI,,," HII NI KAULI YA DR. SLAA

  KATIBU  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amezungumzia video aliyorekodiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare na kusema ni ya kutungwa na vyombo vya dola.

Dk. Slaa pia amelituhumu Jeshi la Polisi kufanya mchezo mchafu kwa maslahi ya kisiasa.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho kufafanua suala la kushikiliwa kwa Lwakatare.

CHADEMA WALITAKA JESHI LA POLISI LIMCHUNGUZE LWAKATARE BILA UPENDELEO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kilikuwa na taarifa za mapema juu ya uwepo wa mkakati unaoratibiwa na kufanikishwa na maafisa wa ngazi za juu wa usalama wa taifa wa kukihusisha chama hicho na njama za kumdhuru mwenyekiti wa jukwa la wahariri Absalom Kibanda ili kukidhofisha chama hicho kisiasa.

Magazeti ya leo Ijumaa ya 14th March 2013

                  
                                                

DIAMOND AMTIA MIMBA PENNY NA KUAMUA KUMZAWADIA GARI LA MILIONI15

 Kupitia segment ya U Heard ya XXL Clouds FM na Soudy Brown, mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa bongo alieandikwa sana kwenye internet mwaka 2012 amethibitisha kumnunulia mkoko mama watoto wake mtarajiwa.

Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa sasa ni mjamzito.

Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari gani anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja kwa hiyo sasa hivi anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”

Alipoulizwa kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu “siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “

Thursday, March 14, 2013

POLISI WAMEMKAMATA KIONGOZI WA CHADEMA, LWAKATARE NA KUMPELEKA MAKAO MAKUU KWA MAHOJIANO

Wilfred Lwakatare ameitwa Makao Makuu ya Polisi sasa hivi kwa mahojiano na jeshi hilo kufuatia video clip iliyowekwa mitandaoni ikionesha  jinsi  alivyokuwa  akipanga  mbinu  za  utekaji....

WILLIFRED LWAKATARE  NI MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA WA CHADEMA...

Kwa taarifa ni kuwa atawakilishwa na wakili Nyaronyo Kicheere na baadaye kama watafungua kesi watakuwa na Mabere Marando.
Je, hii sio double standard ndani ya taifa?
Mbona Mwigulu hajakamatwa baada ya kusema ana mkanda wa njama za kufanya mauaji?

MAELEZO YOTE NI KWA HISANI YA JAMII FORUM

HATIMAYE PAPA MPYA APATIKANA HUKO VATICAN

  Jorge Mario Bergoglio(Pope Francis) akipewa salamu na Papa aliyejiuzuru Benedict 16

Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa. Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I. Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.

 Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao. Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki. Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.

Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya. Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.

Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne. Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa

Magazeti ya Leo Alhamisi ya 14th March 2013





Wednesday, March 13, 2013

MATOKEO MECHI YA BAYERN VS ARSENAL MARCH 13




                                     


"MAPOZI" YA LULU MICHAEL AKIWA KITAA...


LULU USO KWA USO NA MAMA YAKE KANUMBA KWENYE KABURI LA KANUMBA

                    Pichani ni Elizabeth Michael/Lulu na Mama mzaz wa Marehemu Steven Kanumba

Magazeti ya leo Jumatano ya 13th March 2013





WEMA SEPETU AAMUA KUZITIA MKASI NYWELE ZAKE...

Mrembo na Miss Tanzania wa zamani, Wema Sepetu ameamua kubaki natural baada ya kuzinyoa nywele zake. Kupitia Instagram, Wema ameshare picha hizo na kuandika, ‘me apa nimenyoa nywele’. Ingia ndani kusoma maoni aliyoyapata baada ya kunyoa.

MOSHI MWEUSI WAFUKA VATICAN KUASHIRIA KUWA BADO PAPA HAJAPATIKANA....

Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye  dohani huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.

Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana  ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.

Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.

Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.

Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi  mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Huyu Ndio Msanii Anaye Ongoza Kulipwa Hela Nyingi Kutokana na Ringtones za Simu

Mwanzilishi wa kampuni ya Push Mobile inayohusika na uuzaji wa miito ya simu, ringback tone (RBT) amesema Diamond ndiye msanii wa Bongo Flava anayeingiza fedha nyingi zaidi.

Shamte ametoa taarifa hiyo jana alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la mchango wa technolojia ya habari na mawasiliano ICT kwenye tasnia ya muziki nchini katika kituo cha ubunifu wa technolojia hiyo cha KINU jijini Dar es Salaam