Saturday, May 4, 2013
Friday, May 3, 2013
UPDATE: MATOKEO YOTE YA KIDATO CHA NNE 2012 YAMEFUTWA NA YATASAHIHISHWA UPYA
Habari kutoka bungeni ni kwamba matokeo yote ya kidato cha nne yamefutwa na yatasahihishwa upya ( Re -grading ) haraka iwezekanavyo..
Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne imesomwa bungeni leo na mh.LUKUVI.
LUKUVI amesema sababu zilizosababisha wanafunzi wafeli ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na utaratibu mbovu wa baraza la mitihani uliotumika bila kuwashirikisha wadau wa elimu
Mh. LUKUVI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS. ...
Hivyo basi, matokeo hayo YAMEFUTWA na MATOKEA YATAFANYIWA RE-GRADING

NEEMA KWA WALIOFELI FORM 4:..MARKS ZAO ZITAPANGWA UPYA
TUME ya kuchunguza sababu za kufeli kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mitihani ya kuhitimu mwaka 2012 imekamilisha kazi yake na taarifa za uhakika zilizolifia gazeti hili zinasema , upangaji alama zao utafanyika upya.
Kama ambavyo gazeti hili lilivyobaini katika uchunguzi wake wa kiuandishi kwamba kulifanyika mabadiliko ya utoaji alama kwa ajili ya mitihani waliyofanya wanafunzi mwaka huo (2012) bila maandalizi kwa wadau, tume hiyo imependekeza alama zipitiwe upya (regrading).
Katika alama za awali, alama D anapoyopewa mtahiniwa baada ya mtihani wake kusahihishwa ilikuwa ni kuanzia alama 21 kwenda mbele na F ilikuwa 20 kushuka chini lakini katika mabadiliko yaliyoleta ‘maafa’ ya kufeli kwa watahiniwa wa mwaka jana, alama D ilianzia 35 na kuendelea, wakati ile ya kufeli (F) ilianzia alama 34 kushuka chini.

FIFA YAWARUDISHA MALINZI NA WAMBURA KUGOMBEA TFF
Kuna taarifa kwamba wagombea wawili, Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa kutoka ndani ya TFF zimeeleza, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeandika barua ambayo imeshatua Fifa tayari kuwarejesha Malinzi, Wambura na wengine waliokuwa wanagombea.
Uongozi wa TFF unatarajia kuzungumza muda mfupi ujao kuanzia sasa katika ofisi zake katika eneo la Ilala jijini Dar es Salaam.
Tayari Salehjembe ametega masikio kuhusiana na kitakachotokea na atatutaarifu kama ni hiki kutoka ndani au kutakuwa na mabadiliko.

"TANZANIA NI MUHIMU KULIKO CHADEMA.....SIPO TAYARI KUSUSIA MCHAKATO WA KATIBA".....HAYA NI MAJIBU YA PROFESA BEREGU KWA DR SLAA
Kutoka Raia Mwema:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,huku yeye akiweka msimamo wake wazi kwamba Tanzania ni muhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.
Habari zilizoppatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, alimwiita msomi ambae ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe. Ndani ya Tume hiyo kwasababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.
Profesa Beregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya kiingereza, "If I am told to choose between my country and my party (Chadema), I will choose my country", akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha Chadema, angechagua nchi yake kwanza.

MASWALI MATANO ALIYOULIZWA GADNER G KUHUSIANA NA WOSIA WA KIFO CHA LADY JAYDEE
Jana Lady Jaydee alitoa wosia akidai kuwa SIKU AKIFA RUGE wa CLOUDS fm asiguse katika mazishi yake na Radio Clouds Fm isithubutu kutangaza wala kutia neno lolote katika msiba huo......
Gadner G ameamua kuvunja ukimya na kuufafanua wosia huo kupitia TBC FM wakati alipohojiwa na mtangazaji Dan Chibo katika kipindi cha The Takeover na haya ndo mazungumzo yao...
Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?

Thursday, May 2, 2013
SHANGWE ZA BAYERN MUNICH DHIDI YA BARCA, NA ZA MECHI PIA.
Thomas Muller akiongoza shangwe za ushindi dhidi ya Barcelona, hapa
ilikua ni mbele ya mashabiki wa Bayern waliosafiri kutoka Ujerumani
mpaka Hispania.
KATIKA SIKU YA MEI MOSI SERIKALI YATANGAZA KUPUNGUZA KODI KATIKA MISHAHARA
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akishikana mikono na viongozi wengine kuimba wimbo wa Mshikamano Daima wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya jana.
Wafanyakazi nchini watapata nafuu kimapato, pale Serikali itakapoanza kutekeleza azma yake ya kupunguza kodi kwenye mishahara (PAYE) wiki mbili zijazo.
Rais Jakaya Kikwete, jana aliashiria hivyo baada ya kutangaza punguzo la PAYE, kwa lengo la kupunguza mzigo wa ugumu wa maisha kwa mfanyakazi.
Alitangaza hatua hiyo alipohutubia wananchi jana katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, yaliyofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kutangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari.
“Tangu mwaka 2007 baada ya kilio cha wafanyakazi, tulipunguza kodi kutoka asilimia 18 hadi 15, na kwa mwaka 2010/11 tulipunguza hadi asilimia 14.

CCM WAMVAA MKUU WA MKOA WA ARUSHA.....WANADAI AMEMUONGEZEA UMAARUFU GODBLESS LEMA
VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Wabunge hao waliliambia gazeti hili mjini Dodoma kuwa kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Lema kwa shinikizo la mkuu huyo, itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo cha kesi ya Lema na hatimaye kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na kubaini kuwa hulka
za utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali zinawapa sifa na umaarufu zaidi CHADEMA.
“Mimi sitaki kuingilia kesi, lakini ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video ya vurugu za Chuo cha Uhasibu Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika eneo la tukio na kuondoka, utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo ambao leo unamfanya Lema aonekane shujaa.
“Leo tunaingia kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani pale Arusha, tunaweza tukashinda, lakini tutafanya kazi ya ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,” alisema Lugola.

"SIJAJA BONGO KUFUATA PENZI LA DIAMOND"...AVRIL
Jana ilikuwa ni birthday ya msanii wa Ogopa Djs ya Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril ambaye alitua jijini dar es salaam juzi na sababu ya ujio wake ilikuwa ni vitu vikubwa viwili.
Akihojiwa katika kipindi cha XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa bongo kwanza ni ku-celebrate birthday yake na fans wa Tanzania, na pili ni ku-launch single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yuko ziarani barani Ulaya, party ilifanyika usiku wa kuamkia jana (April 30) pale Elements club.
Kuhusiana na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina yake na Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya Kesho, Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote kati yangu na diamond na sijaja Tanzania kufuata penzi lake... we are just friends na relationship yetu ni proffesional relationship katika muziki", alisema Avril.
Hii ndo birthday party ya kwanza kwa Avril kufanya, birthdays zake zote zilizopita alikua anasheherekea kwa kuchill tu nyumbani na familia yake.

WABUNGE WATWANGANA NGUMI NDANI YA BUNGE...
Bunge la Venezuela.
Makonde yameibuka bungeni na baadhi ya wabunge kujeruhiwa katika sintofahamu, kutokana na mjadala kuhusu uchaguzi wa hivi karibuni unaobishaniwa.
Upande wa upinzani ulisema juzi kwamba wabunge wao saba, walishambuliwa na kujeruhiwa wakati wakipinga hatua ya kuwazuia kuzungumza katika Bunge hilo, kutokana na kukataa kwao kutambua ushindi wa Rais Nicolas Maduro uliofanyika Aprili 14.
Wabunge wa chama tawala walilaumu wapinzani wao hao na kuwaita mafashisti kwa kuanzisha vurugu, hali iliyoonesha siasa tete katika Taifa hili mwanachama wa OPEC baada ya kifo cha Msoshalisti, Hugo Chavez mwezi jana.

"SIKU NIKIFA RUGE MUTAHABA NA KUSAGA WASIHUDHURIE MAZISHI YANGU"....LADY JAYDEE
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Subscribe to:
Posts (Atom)