Msanii M2 the P aliyekutwa mahuhuti pamoja na Ngwair ambaye alifariki, anaendelea vizuri kiafya na ameshatoka hospitali. Mpaka sasa M To The P hajui kama Mangwea amefariki na anadhani mwenzake ametangulia kwenda Dar es Salaam.
M2 the P alipotembelewa na huyu sister anayeitwa Magie aliyeenda kumjulia hali baada ya msanii huyo kutoka hospitali M2 the P alipotembelewa na huyu sister anayeitwa Magie aliyeenda kumjulia hali baada ya msanii huyo kutoka hospitali m2-the-p
"Hapo Magie anamtania ikabidii amyeyushe eti ukirudi bongo mwambie
Mangwea nina case nae yakuondoka bila kuniaga. Dah so so sad"- Jestina
George “Hapo Magie anamtania ikabidii amyeyushe eti ukirudi bongo
mwambie Mangwea nina case nae yakuondoka bila kuniaga. Dah so so sad”-
Jestina George Magie amekuwa karibu sana na M2 The P na alikua karibu na
marehemu Albert “Ngwair” Mangwea kwa muda waliokuwa Africa Kusini. kama
inavyoonekana pichani,
Magie alienda kumcheki M2 The P, kumpa moyo
na kumchangamsha. Alipo fika alimkuta M2 The P amejawa na mawazo huku
kikombe chake cha chai kiko mezani ikabidii aanze kumtania tania angalau
aondokane na mawazo. Bado anamuuliza rafiki yake kipenzi Mangwea maana
hajui yaliyo mfika. Tuendelee kumuombea M2 The P maana ana mtihani
mkubwa mbele yake akija kujua ukweli, na ni Mungu pekee ndo ataweza
kumsaidia.
Thursday, June 6, 2013
VYAMA VYA UPINZANI VYANUIA KUUNGANA 2015
Vyama vya siasa vyenye idadi ndogo ya wanachama nchini vimekubali hatua ya kuungana na kuwa Muungano wa vyama (Alliance) kwa lengo la kupata nguvu ya uwakilishi wa kuingia katika Bunge Jipya la Shirikisho baada ya rasimu mpya kupitishwa kwa ajili ya uchaguzi ujao.
Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kutangaza rasimu iliyotoa mwelekeo wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania.
Akizungumza jana na gazeti la Mwananchi, Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza amesema hali hiyo inaweza kuleta changamoto kubwa hivyo muda sahihi wa vyama vichanga kuzungumzia hili ni sasa.
Katibu mkuu wa chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabi anaunga mkono hatua ya kuunganisha vyama hivyo kwa lengo la kuwakilisha mawazo yao kwa maslahi ya taifa.

MUME WA KHADIJA KOPA AFARIKI DUNIA
Khadija Omar Kopa akiwa na mumewe Jaffari Ally enzi za uhai wake.
Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya Bagamoyo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

PICHA TOKA MOROGORO AMBAKO MWILI WA ALBERT NGWEA UMEPOKELEWA TAYARI KWA MAZISHI
Msafara wa kupokea mwili wa msanii marehemu Albert Mangwea ukiwa unaingia morogoro hapa ni eneo la nane nane,Umati mkubwa umejitokeza katika mapokezi mpendwa wao
Wednesday, June 5, 2013
"SITANYAMAZA KUSHAMBULIWA KWANGU.NI LAZIMA JAMII IJUE"...HII NI KAULI YA KIBANDA BAADA YA KURUDU TANZANIA
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda (wa tatu kulia) akiwasili jana.
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda amerejea chini jana kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa na kusisitiza kwamba hatanyamaza kuzungumzia janga la kushambuliwa kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Kibanda alisema asingependa kuona jambo hilo linamtokea mwandishi mwingine wa habari.
Kibanda, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alikuwa akitibiwa huko baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5, mwaka huu.

Monday, June 3, 2013
HUTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JUNE 3, 2013
HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE, DAR ES SALAAM.
UTANGULIZI
Ndugu Wananchi,
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.
Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga. Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.

ALBERT MANGWEA AAGWA NA WATANZANIA WALIOKO AFRIKA KUSINI.....MWILI WAKE UTALETWA KESHO SAA NANE
Watanzania waishio nchini South Africa wamepata nafasi ya kuuaga mwili
wa Albert Ngwea kuelekea katika safari ya mwisho wakiongozwa na Msanii
Bushoke na Mtoto wa Mhe. Kingunge Ngombale mwiru, Kinjeketile
wanaosimamia mipango ya kuaga mwili nchini Afrika kusini...
Mwili wa marehemu utaletwa Tanzania kesho saa nane.....

MSHIRIKI WA TANZANIA ( FEZA KESSY) KATIKA BIG BROTHER YUKO HATARINI KUTOLEWA...KURA ZAKO ZINAHITAJIKA
Kama hisia za wengi zilivyokuwa kuhusiana na Betty kulipiza kisasi, mambo yameenda hivyo..Betty ambaye ni Head of House wa Diamond house amemuokoa Bolt na kumuweka kikaangoni Feza..Katika Ruby house, Selly ambaye ni Head of house huko, naye ametumia ukuu wake wa kaya kumuokoa Biguesas na kumtia kitanzini Koketso..Wiki hii Feza, Dillish, Hakeem, LK4 na Koketso wako kikaangoni..Wakati wa kupiga kura kwa nguvu zote umewadia.. Kazi kwetu watanzania kumpigia kura wakwetu..Tuwahimize pia marafiki zetu Africa kumpigia kura Feza kwani kura zao ni muhimu sana.. -- Kila nchi inahesabiwa kama kura moja.
Kupiga kura tembelea --> http://bigbrotherafrica.dstv.com/vote/

NEYMAR ATUA RASMI BARCELONA
Klabu ya Barcelona imemtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Neymar
da Silva Santos Júnior 'Neymar' klabuni hapo kwa mara ya kwanza kwa
ajili ya kuanza kuitumikia timu hiyo. Pichani juu ni baadhi ya taswira
za mchezaji huyo akiwasili klabuni hapo.
GARI LA WEMA NYANG’ANYANG’A
GARI la Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ limepata ajali na kuwa nyang’anyang’a huku dereva aliyekuwa akiliendesha akiumia vibaya.

Gari la Wema kwa ndani baada ya ajali hiyo.
Habari zilisema kuwa ajali hiyo ilitokea maeneo ya Morocco, Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo dereva huyo ambaye inadaiwa ni ‘jamaa wa Wema’ aliyetajwa kwa jina moja la Robby aliumia mguu wa kushoto na taya hivyo kukimbizwa hospitali (jina halikupatikana mara moja).

KAMATI YA NGWEA YAKUSANYA MILIONI 32....MAMA MZAZI APANDWA NA PRESHA BAADA YA MWILI WA NGWEA KUZUIWA HUKO AFRIKA KUSINI
KAMATI ya Mazishi ya aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva, Albert Mangwea ‘Ngwea’, mpaka jana mchana ilikuwa imekusanya jumla ya Sh milioni 32 kutoka kwa wadau mbalimbali.
Kamati hiyo inahitaji Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini mpaka Morogoro kwa ajili ya mazishi. Fedha hizo pia zinahitajika kwa ajili ya kuratibu shughuli nzima ya mazishi.
Mangwea alifariki dunia Jumanne iliyopita nchini Afrika Kusini akiwa usingizini kwa madai ya kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya.
Alitarajiwa kuwasili nchini jana lakini kushindwa kutoka kwa ripoti ya uchunguzi wa madaktari kwa wakati, kumesababisha isijulikane atatua lini, licha ya kudaiwa kuwa anaweza kutua leo.
Kamati ya Mazishi bado inaendelea na mchakato wa kuratibu shughuli hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu akiwa Mbezi Goig jijini Dar ambako ndiko kwenye msiba huo, mmoja wa waweka hazina wa kamati hiyo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, alisema mpaka sasa kamati yake imefikisha Sh 32,259,000 ingawa wanatarajia kuendelea kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau.
Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa michango yao katika msiba huo ni P-Funk aliyetoa Sh milioni tano, Clouds Media Group (Sh milioni tano) na Push Mobile (Sh milioni tano).
Juzi Kampuni ya Global Publishers ilitoa Sh milioni moja.
“Nawasisitiza Watanzania waendelee kutoa michango yao kwa ndugu yao ili kuonyesha umoja tulionao. Fedha zikiwa nyingi tunataka kumfanyia kitu mama yake ili kuendelea kumfariji kwani kipindi hiki ni kigumu kwake,” alisema P-Funk.
Wakati huohuo jana taarifa zilisema mama mzazi wa Mangwea aishie Morogoro, Denisia Mangwea, alipandwa na presha baada ya jana kupata taarifa kuwa mwili wa mwanaye umezuiwa Afrika Kusini kutokana na uchunguzi wa madawa ya kulevya. Alikimbizwa hospitali na inadaiwa anaendelea vizuri.
Mangwea aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa kali zikiwemo Gheto Langu, She Got a Gwan, Mikasi na Tupo Juu.

Friday, May 31, 2013
TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA HII HAPA
Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda
TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA IMEWASILISHWA NYUMBANI HOTEL – TANGA MEI 30, 2013
UTANGULIZI:Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.
Tukio hilo liliishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa ujumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lilomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madkatari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.

Subscribe to:
Posts (Atom)