Monday, June 10, 2013

Makamu Wa Rais Akutana Na Kibanda

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhariori wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, AbsalomKibanda, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 10, 2013 kwa mazungumzo. Kibanda alimtembelea Mhe. Makamu ili kumwelezea hali yake kiafya inavyoendelea baada ya matibabu. Picha na OMR

Magazeti ya leo Jumatatu 10th June 2013

 




STAR TV YATANGAZA KUJITOA KATIKA VING'AMUZI VYA STAR TIMES......TCRA YAGOMA NA KUDAI KUWA SHERIA HAIRUHUSU KUJITOA

BAADA ya Televisheni ya Star TV kutangaza kujitoa kurusha matangazo yao kupitia kingamuzi cha Star Times, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema sheria na leseni ya huduma, inazuia kuchukua hatua hiyo.

Hata hivyo, TCRA imesema inafanya uchunguzi na leo itakutana na uongozi wa Star TV na Star Times, kuzungumzia suala hilo ili hatua za udhibiti, zichukuliwe kuwezesha wananchi kupata haki ya msingi ya kupata matangazo ya kitaifa kupitia televisheni hiyo.

Star TV walitangaza kutoonekana kupitia Star Times siku chache zilizopita. Uchunguzi wetu umebaini kuwa, jana waliwasilisha barua ya hatua hiyo kwa kampuni ya Star Times kupitia mwanasheria wa kampuni yao.

Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy aliliambia HabariLeo  jana kuwa na wao wamesikia taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari Lakini, alisema Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, haitoi fursa kwa watu wenye televisheni kujitoa ama kujiweka kwenye ving’amuzi watakavyo.

Saturday, June 8, 2013

Magazeti ya leo ijumaa 8th June 2013





CHADEMA WAUNGA MKONO RASIMU YA KATIBA MPYA

 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema chama chake kinaunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyotolewa na Jaji Joseph Warioba.

Mwenyekiti huyo alikuwa akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji la Mbeya katika mkutano wa kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Iyela kwa tiketi ya Chadema Charles Nkelwa.Kiongozi huyo wa upinzani bungeni amesema sababu kubwa ya kuunga mkono rasimu hiyo ni kwamba mambo mengi yaliyoorodheshwa na chama hicho yamekubaliwa.

Mbowe amesema jambo kubwa lililofanyiwa kazi ni kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika. Mbowe amesema amesikitika kuona baadhi ya wanaCCM wakiipinga serikali ya Tanganyika na kung'ang'ania serikali mbili na kudai watu hao ni wanafiki wanaopaswa kupuuzwa na wananchi.

Kauli ya Mbowe imekuja wakati ambapo mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dr Kitila Mkumbo alinukuliwa kusema rasimu mpya ya Katiba iliyotolewa na Warioba ni bora mara mia mbili akilinganisha na katiba ya sasa.Mara baada ya mkutano huo maelfu ya watu walitanda barabarani kumsindikiza kiongozi huyo anayependwa sana jijini Mbeya.

MFULULIZO WA VIFO VYA WASANII WAMFANYA DOKII AFUNGUKE KUWA NI MUNGU ANAWAADHIBU

MWIGIZAJI Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ameibuka na kusema kuwa vifo vya wasanii vimetokea kutokana na kujisahau hivyo Mungu ameamua kuwaadhibu.

Akiongea na mwandishi wetu katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu ambapo mwili wa Mangwea ulikuwa ukiagwa, Dokii alisema matukio ya vifo vya wasanii mbalimbali yaliyotokea miaka miwili mfululizo ni pigo kubwa kwani wengi ni vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kitu ambacho anakiona ni ishara kuwa Mungu anataka kujidhihirisha kwa wasanii.
“Wasanii tulijisahau sana na kuona Mungu hayupo kwani kipindi bado hatujatoka na tunatafuta kutoka kisanaa, tulikuwa tunamuomba kila wakati lakini baada ya kutoka na kuwa mastaa tumemsahau kabisa.

“Hatukumbuki kwenda ibadani tunabaki kuendekeza starehe za dunia tu, hivyo tubadilike kwani Mungu ameanza kujionesha kwetu kwamba yupo,” alisema Dokii.

NAIBU WAZIRI WA JINSIA NA WATOTO AIBUA KASHIFA YA RUSHWA YA NGONO KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA

Suala la uwepo wa rushwa ya ngono kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limetinga bungeni.

Suala  hilo Lilijitokeza jana wakati Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), alipomaliza kujieleza bungeni akiomba kura kwa wabunge wamchague awe mjumbe kwenye taasisi hiyo.

Baada ya Mbunge huyo kumaliza kujieleza, alisimama Mbunge wa Viti Maalumu, Naibu Waziri wa Jinsia na Watoto, Ummy Ally Mwalimu aliyemhoji atatoa mchango gani katika kupambana na changamoto kwenye chuo hicho, ikiwamo rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia, ili kusaidia watoto wa kike wasome vizuri.

Kabla ya Mangungu kujibu swali hilo, Mbunge wa Chakechake, Mussa Haji Kombo (CUF), aliomba Mwongozo wa Spika kutaka muuliza swali afute kauli yake kwani ni ya udhalilishaji na inaweza kuleta matatizo.

 Hata hivyo, Spika Anne Makinda aliingilia kati na kusema hakuna haja ya kufuta kauli hiyo kwa vile ndiyo hali halisi iliyopo.

Friday, June 7, 2013

Magazeti ya leo Ijumaa 7th June 2013




KHADIJA KOPA AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE JANA KWA AJILI YA MSIBA WA MUMEWE JAFFARI ALLY

 Khadija Kopa akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za mumewe kufariki.

Akipewa sapoti wakati akielekea uwanja wa ndege.

Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jaffari Ally Yussuf aliyefariki dunia jana alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi.

Thursday, June 6, 2013

HATIMAYE NGWEA AZIKWA KWENYE MAKABURI YA KIBONDA MKOANI MOROGORO....HIZI NDIO PICHA ZA MAZIKO YAKE

 Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.

PICHA ZA M 2 THE P AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI WA KUMUAGA ALBERT NGWEA MOROGORO MCHANA HUU

M2  THE P amefanikiwa  kutoa  salamu zake  za  mwisho  kwa  rafiki yake  kipenzi  ambaye  alikuwa  naye  huko  Afrika  kusini  tena  walikuwa  ndani  ya  chumba  kimoja  kabla ya  mauti  kumkuta Ngwea....!!

Mwanzoni, M 2 THE P alikuwa  amefichwa  na  kudanganywa  kuwa  Ngwea  alikuwa  ametangulia  Tanzania. Baadaye  Maggie  alilazimika  kumweleza  ukweli......

M 2 THE P AREJEA TANZANIA KUMZIKA MANGWEA LEO

Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya leo (June 6).

Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2 The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake Mangwea.

“Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi, asanteni,” alisema.
Msikilize hapa

Magazeti ya leo Alhamisi ya 6th June 2013