Wednesday, December 31, 2014

HAKIKA WANAWAKE TUNAWEZAAAA "MTUNZI MKONGWE WA VITABU ZANZIBAR AZINDUA VITABU VITATU VYA HADITHI ZA KALE"


 Mtunzi mkongwe wa vitabu Zanzibar Bi. Fatma Moh’d Salim (Jinja) akionyesha vitabu vya hadithi za kale alivyovitunga, katika sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo zilizofanyika nyumbani kwake Chukwani Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa Redio Annur Fm Kasim Khamis akimuuliza suali Bi. Fatma Jinja kuhusiana na utunzi wa vitabu vyake alivyo vizindua.…
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo wakimskiliza Bi. Fatma Jinja (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo juu ya utunzi wa vitabu hivyo .

Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na mtunzi wa vitabu Bi. Fatma Jinja huko nyumbani kwake Chukwani Zanzibar baada ya uzinduzi wa vitabu vyake.

 Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

SHEIKH SHARIF AZUA MAPYA YA URAIS 2015


Sheikh Shariff Matongo  akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)kuhusu  ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka 2015.

Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi.

Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa  ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na  na mwenye kambi katika Chama cha…

Zitto Kabwe kuhusu Serikali kutekeleza maazimio yaliyotolewa na Bunge…

                                                                      Zitto-Kabwe1

Mbunge wa Zitto Kabwe leo amewahutubia Wananchi wa Mtwara kupitia mkutano ulioitishwa na chama cha Wananchi CUF na kutoa ufafanuzi juu ya sakata la account ya Tegeta Escrow.

Akizungumzia sakata hilo Zitto Kabwe amesema kuwa baadhi ya viongozi waliohusika na sakata hilo ambao mpaka hivi sasa hawajachukuliwa hatua yoyote lazima wachukuliwe kwa kuwa serikali haiwezi kupingana na maazimio ya bunge.

“ Utekelezaji wa maamuzi ya Bunge hauna mjadala… sisi kama Wabunge wa Kambi ya Upinzani mwezi January kazi ya kwanza ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya Bunge… Tunachokitaka kila mtu aliyehusika kwenye Escrow ni lazima awajibike…“– Zitto Kabwe.

Sisi lazima tuutumie mwaka 2015 kama mwaka wa uwajibishaji, mwaka wa kuwajibishana… safari hii mmewawajibisha kwenye Seikali za Mitaa, hongereni sana, tunaenda kuwawajibisha kwenye Serikali kuu sasa…”– Zitto Kabwe.

Kanye West na Kim Kadarshian wamenunua nyumba mpya


 Ratiba za mastaa wengi walio katika uhusiano wa kimapenzi huwa zinawafanya wanakuwa busy na kushindwa kupata time ya kuspend pamoja, Kim Kardashian na Kanye West ni moja ya mastaa ambao wao pia ratiba yao huwa ngumu kupata muda wa kukaa pamoja.
 Kim yuko busy na TV show na deal zake za mitindo lakini ratiba yake haimfanyi awe busy kama ilivyo kwa Kanye ambaye amekuwa akizunguka kwa ajili ya show na pia kurekodi nje ya Marekani.

Story ya mwisho kusikika kuhusu mastaa hao ni ile ambayo imetoka siku moja iliyopita, wamenunua nyumba ya jirani yao yenye thamani ya dola mil.3 maeneo ya Los Angeles ambapo mkakati walio nao ni kuikarabati kwa kuweka vitu kadhaa ikiwemo Studio ya kisasa.
Kwenye nyumba hiyo pia kutakuwa na uwanja wa basketball, sehemu ya kuangalia filamu, sehemu ya michezo, chumba cha massage na eneo la kufikia wageni, studio itakayokuwepo hapo huenda ikasaidia kumfanya Kanye apate muda mwingi kidogo wa kukaa nyumbani tofauti na ilivyo sasa.

Tukio hili limetokea leo mahakama ya kisutu Dar es salaam

 Hizi ni baadhi ya picha za tukio hili jamani samahani kwa picha zinazoendelea




Saa kadhaa zilizopita Polisi walimfyatulia risasi mtuhumiwa aliejaribu kutoroka baada ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu Dar es salaam asubuhi ya December 31 2014.

Muda mfupi baadae Polisi ikatoa taarifa kwamba mtuhumiwa wa dawa za kulevya aliyeuwawa ni Abdul Koroma raia wa Sierra Leone na aliuwawa kwa risasi wakati akitoroka Mahakamani.

Wednesday, October 22, 2014

Chanjo ya Ebola Kutolewa Afrika Magharibi

Shirika la afya duniani, WHO limearifu kuwa liko mbioni kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ambao umeripotiwa kuua takribani watu 4,500 huku nchi za Afrika Magharibi zikiripotiwa kuathirika zaidi tangu kulipuka kwa ugonjwa huo.

Taarifa iliyoripotiwa na CNN imesema kuwa shirika hilo limepanga kuanza utekelezaji wa jaribio hilo mapema Januari mwaka 2015 katika nchi za Afrika Magharibi, huku wakisisitiza kuwa chanjo zote hazina madhara kwa afya ya binadamu, japo chanjo hiyo haitowahusu wagonjwa ambao tayari wana maambukizi Ebola.

Mratibu wa zoezi hilo Dk. Marie Paule Kieny amesema, chanjo hiyo itatolewa kwa mtu yoyote atakayekuwa tayari kujitolea kushiriki.

Amezitaja nchi za Mali, Uingereza na Marekani kuwa ni baadhi ya nchi ambazo jaribio la chanjo hiyo litafanyika.

Shirika la afya limesema limeagiza wataalamu kufanya ziara Afrika Magharibi katika nchi ambazo wananchi wake wameathirika zaidi na ugonjwa huo, ambapo pia ziara hiyo itahusisha pia zoezi la ukaguzi wa vituo ambavyo vitatumika kutolea huduma hiyo ya chanjo.

Iwapo chanjo hii itafanikiwa itafufua matumaini kwa watu wa Afrika ya Magharibi ambao wameshuhudia athari kubwa zilizosababishwa na Ebola ambapo watu zaidi ya 4,500 wameripotiwa kufariki na wengine zaidi ya 9,000 wana maambukizi ya ugonjwa huo.

Bilionea wa Madini Arusha auwawa leo So sad jamani

Jamani samahani kwa picha hii ila ndio hali halisi polisi jamani mtandao wa majambazi bado unaendelea kutishia usalama wa wananchi jijini arusha.Poleni wafiwa na wana Arusha secta ya madini. P.I.P Fadhili

Mti uliofufuka huko Tabora haya ni maajabu jamani ?




 
Jamani haya ni maajabu hii imetokea mkoani Tabora mti ulioanguka miaka mitatu iliyopita umesimama huku wanyeji wakisema ulikuwa ukipiga kelele sasa najiuliza ni muujiza wa mungu au nguvu za giza mbona hii ni ajabu jamani mlioko huko tupeni habari kamili.

Tuesday, October 21, 2014

Unaikumbuka Hii....( HATIMAE LUDOVICK AFUNGUKA AELEZEA UHUSIANO WAKE NA LWAKATARE NA MWIGULA)

*Aelezea uhusiano wake na Mwigulu, Lwakatare

*Asema yeye bado ni mwanachama hai wa Chadema, amkwepa Kibanda
SIKU chache baada ya Mahakama kumuachia kwa dhamana mshitakiwa mwenza wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovick, amefunguka na kuelezea tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, ikiwamo uhusiano wake na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake.

Maswali na majibu yake ilikuwa ni kama ifuatavyo;

Asante Mungu u Mwema


 Nakupenda  baby wangu mungu akupe maisha marefu na afya njema Happy birthday my Precious 1yrs old Asante mungu

Thursday, October 9, 2014

Hongera my pacha

Mungu awalinde awajalie upendo na uvumilivu hakika mmependeza sana

Hahahah

Pendeza sisi chezea posiiii duu naanza mazoezi kwa kweli ufupi umezidi sasa hahahahahahahaaa

Hi wapenzi wa Tanzania asilialive.blogspot .com

Habari za siku nyingi wapenzi wa tanzania asilialive kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu tunaomba radhi kutokuwepo hewani kwa muda mrefu.kwa sasa tunajaribu kurekebisha na punde tutakuwa hewani kuendeleza libeneke hili.

Asanteni sana by  faulisa

Sunday, June 22, 2014

Breaking News, Ajali iliyoua sita leo Dar es salaam.



Watu sita wamefariki papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya iliyohusisha magari manne iliyotokea eneo la Makongo karibu na hospitali ya Lugalo Dar es salaam.

Baadhi ya mashahuda wa ajali hii wamesema kuwa imesababishwa na uzembe uliofanywa na dereva wa daladala iliyokuwa ikitoka Tegeta kwa kupita upande usio wake.

Tuesday, May 6, 2014

jamani bomu tena kanisani jijini mwanza

Bibi Benadta alifred ajeruhiwa vibaya baada ya kufungua kitu asichokijua baada ya kukaa kwa muda sehemu ya kupumzikia eneo la kanisa hilo jijini mwanza. habari kamili na picha tunakuletea hivi punde..