Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa katika Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Katika Salamu zake, Naibu Katibu Mkuu ameelezea kuguswa kwake na tukio la ajali ya kuzama kwa meli na hasara iliyotokana na ajari hiyo ikihusisha pia kupotea kwa maisha ya watu. Mhe. Jan Eliasson ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu zao za pole na kuungana na watanzania katika kipindi hiki cha majonzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akizungumza na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ambapo alielezea namna gani anavyoifahamu Tanzani na mapenzi yake makubwa kwa nchi hiyo na kwamba ni kama miaka miwili tu iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar. Katika salamu zake za pole Mhe. Elliasson amesema sala na dua zake anazielekeza kwa wahanga wa tukio hilo, Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja na watanzania katika kipindi hiki kigumu.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Mhe. Jan Eliasson ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufutia ajali ya kuzama kwa meli iliyotokea hivi karibuni.
Katika salamu zake ambazo amezitoa wakati akisaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Naibu Katibu Mkuu amesema, ameshtushwa na kuguswa sana na taarifa za tukio la kupinduka na hatimaye kuzama kwa meli, tukio ambalo limesababisha kupotea kwa maisha ya watu.
“ Ninapenda kutoa salamu zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wa pande zote mbili. Nimeguswa sana na taarifa hizi, sala na dua zangu zinakwenda kwa wahanga wote wa tukio hili. Mimi Binafsi na Umoja wa Mataifa tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ” Amesema Naibu Katibu Mkuu.
Katika mazungumzo yake na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu, Mhe. Jan Eliason amesema anaifahamu vema Tanzania na kwamba miaka miwili iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.
“ Ninaifahamu vizuri sana Tanzania, nimefanya kazi kwa karibu sana na Dkt. Salim Ahmed Salim, bado ninakumbukumbu nzuri sana za Tanzania. Na nililikuwa kisiwani Zanzibar kama miaka miwili hivi iliyopita. Kwa kweli tukio hili limenigusa sana”. Akasema Naibu Katibu Mkuu raia wa Sweden ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika nafasi iliyoachwa na Dkt. Asha-Rose Migiro.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika hapa Ubalozini kutoka salamu zao za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwa Watanzania wote .
Saturday, July 21, 2012
14 Wauawa Katika Shambulizi Marekani
Ukumbi wa Sinema mjini Denver
Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji ya watu kumi na wanne mjini denver huko colorado.
Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la Aurora wakati huu mgumu.Alikiri kuwa serikali itakahakikisha aliyehusika anakamatwa.
Mtu mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa barakoa aliwauwa kwa kuwapiga risasi watu hao kumi na wanne na kuwajeruhi takriban hamsini wakati wa onyesho la filamu ya Batman,The Dark Knight Rises.
Walioshuhudia tukio hilo kwenye kitongoji cha mji huo cha Aurora walisema mtu huyo aliyekuwa amevalia kifaa cha kujikinga dhidi ya gesi aliingia ndani ya ukumbi huo na kurusha gesi ya kutoa machozi. Pindi gesi ilivyojaa kwenyen ukumbi huo mshukiwa akaanza kuwafyatulia waliokuwemo risasi.
Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

YANGA SASA INATISHA, YAWACHAPA APR 2-0 KAMA WAMESIMAMA,
Kikosi cha Yanga
Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Nizar Khalfan.
Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Rashid Gumbo, Shamte Ally, Jerry Tegete, Juma Seif, Idrissa Assenga, Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo na David Luhende.
Kocha; Tom Saintfiet (Ubelgiji)
Kikosi cha APR
A.P.R.; Jean Claude Ndoli, Mbuyu Twite, Kabange Twite, Mugiraneza Jean, Leonel St Preus, Johnson Bagoole, Iranzi Jean Claude, Ngabo Albert, Tuyizere Donatien, Suleiman Ndikumana na Olivier Karekezi.
Benchi; Ndayishimiye Jean, Kwizera Ernest, Habib Kavuma, Mubumbyi Barnabe, Ngomirakiza Herman, Danny Wagaluka na Sekamana Mzime.
Kocha; Ernest Brandy (Uholanzi).
Kocha wa APR, Ernest Brandy kulia akiwa na kocha wa Yanga, Tom Saintfiet kabla ya mechi
Kiiza akiwa amembeba juu Bahanuzi kumpongeza
Yanga imechukua ushindi wa goli mbili bila kwenye mechi ya Jana na APR magoli yaliyofungwa na Said Bahanuzi kwenye dakika ya 23 na 67.
Kwa idadi hiyo ya magoli, Bahanuzi anatimiza magoli manne toka michuano ya Kagame ianze.
APR walibadilika kwenye kipindi cha pili na kulishambulia goli la Yanga pasipo mafanikio ya kufunga pamoja na nafasi nzuri walizopata, Kama goli la dakika ya 43 la Yanga lisingekataliwa basi Yanga ingeondoka na ushindi wa 3-0.

Friday, July 20, 2012
UZINDUZI WA KAMPENI YA UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI WA KIKE KWA SHULE ZA SEKONDARI.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.Ummy Mwalimu (MB) akicheza ‘kwaito” na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kibaigwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike kwa shule za sekondari.
Mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Mh. Susan Lyimo(MB) akiongea katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji ujenzi wa wa mabweni- Kibaigwa Katika hafla hiyo jumla ya shilingi 37,214,000/= zilipatikana ikiwa ni ahadi na fedha taslim.
Dk. Naomi Katunzi Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) akimkabidhi, Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) mkasi kwa ajili ya kuzindua rasmi harambee ya ujenzi wa mabweni wanafunzi wasichana wa shule za sekondari nchini.
Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kibaigwa Mh Job Ndugai (MB) Akivuta utepe uliokatwa na mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu huku tukio hilo likishangiliwa na wananchi wa Kibaigwa.
Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Sylvia Lupembe Gunze (kushoto) akijadiliana na Diwani wa Kibaigwa Mh.Richard Kapinye na Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Kongwa BiBI Emilia Litunguru.
Mjumbe wa Bodi ya soko la Kibaigwa, Bibi Asha Rajab akitoa ahadi ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Kibaigwa. Bodi iliahidi kuchangia shilingi milioni 6 katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa Mabweni inayoendeshwa na TEA.
Mgeni Rasmi Mh. Ummy Mwalimu (MB) akitoa mchango wake na akihimiza watu wengine wachangie katika Kampeni ya ujenzi wa Mambweni.
Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa Mh.Job Ndugai (MB) akiongea na wananchi wa jimbo lake pamoja na wageni mbalimbali waliohudhulia uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana. Shule ya Sekondari Kibaigwa itafaidika na mpango huo.

Hongera Teresea Na Glory kwa kupata Sakramenti ya Pili (Kumonyo)
Hakika ni atua nyingine katika maisha hasa ya kiroho mungu awape hekima na maarifa kiakili, kimwili na kiroho nitawalea ipasanyo kama mama mlezi.nawapenda sana.
Wakaka na Dada zao wakipozi
Mama mzazi akiwa na wazimamizi wa wanae big up sana my sister umekuza madinti.
Mabrother
Wageni wakiwa nyumbani wakiwasubiri mabibi harusi wetu. namuona mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa, wifi langu mama mwalimu na marafiki zangu wakibadilishana mawili matatu watu raha bwana kukutana.
Sherehe imekwisha jamani asanteni mashostito mmenitia joto mungu awabariki sana

UAMUZI KUHUSU SUALA LA MCHEZAJI KEVIN YONDANI
mchezaji Kevin Yondani ni la kiutendaji, hivyo uamuzi wa Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na Klabu ya Simba kwa suala hilo la kiutendaji kama Sekretarieti ilivyofanya katika barua yake ya Julai 14 mwaka huu ulikuwa sahihi.
2. Kamati ilibaini kuwa Mkataba wa mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba ulimalizika Mei 31 mwaka huu. Hivyo kwa taratibu za usajili mchezaji Kevin Yondani kuanzia Juni 1 mwaka huu alikuwa ni mchezaji huru.
3. Aidha Kamati ilibaini kuwa Mkataba uliowasilishwa na Klabu ya Simba TFF ukiwa na maana ya kuongeza mkataba uliokuwepo TFF baina ya mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba uliwasilishwa TFF, Juni 7 mwaka huu ambapo ni kinyume cha utaratibu wa kuongeza mikataba ya wachezaji unaozitaka klabu kuwasilisha mikataba ya kuongeza muda wa mikataba ya wachezaji wao wakati mkataba halisi haujaisha muda wake. Hivyo mkataba huo kwa jicho la kisheria haupo.
4. Hata kama kamati ingeuona mkataba huo katika jicho la sheria, bado mkataba huo una tatizo la kisheria hasa katika tarehe ambazo pande mbili husika ziliingia makubaliano hayo. Ukiuangalia mkataba huo unabainisha kuwa, wakati mchezaji Kevin Yondani aliingia makubaliano Desemba 23 mwaka jana, upande wa pili wa kimkataba ambao ni Klabu ya Simba inaonekana iliingia makubaliano hayo kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Geofrey Nyange Kaburu, Desemba 23 mwaka huu.
5. Kisheria utata huu unaweza kuondolewa na pande husika tu kwa kurekebisha dosari hiyo kwa maridhiano kuweka saini katika mabadiliko hayo ili kuthibitisha mabadiliko hayo. Hivyo katika jicho la kisheria mkataba huo hauwezi kutumika kumzuia mchezaji huyo kwenda katika klabu anayoipenda wakati akiwa huru.
Kutokana na maelezo yote hapo juu, Kamati imeridhia hatua iliyochukuliwa na Sekretarieti ya TFF ya kumruhusu mchezaji Kevin Yondani kuichezea timu ya Yanga katika mashindano ya Kombe la Kagame 2012.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Rais Kikwete Na Mama Salma Kikwete Watua Zanzibar Kutoa Rambirambi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza Bw. Kitwana Makame Haji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya meli waliolazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja mjini Unguja Jana Jioni.
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole Bi Salome Abeli, mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission jijini Arusha, aliyekuwa njiani kuelekea Pemba kikazi kabla ya kupatwa na ajali hiyo ya meli. Amesema hali yake inaendelea vyema hapo katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita mbele ya miili ya waliokufa katika ajali hiyo ya meli jana karibu na kisiwa cha Chumbe. Hapa ni uwanja wa Maisara ambako miili huletwa kwa kutambuliwa.

Subscribe to:
Posts (Atom)