Friday, July 27, 2012

Kaburu Anahatia Kupanga Kumuua Mandela

Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.

Mahakama ya Pretoria ilimpata kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora alipatikana na hatia ya kupanga kummua Mandela mwaka 2002.

Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.

Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 Afrika kusini.

Wachanganuzi wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana katiki ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.
Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.
Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.
 Chanzo:  http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Makamu Wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal Atembelea Chuo Kipya Cha Nelson Mandela

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Chuo kipya cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila,  leo Julai 27, 2012 akitembelea mazingira ya Chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni kilichopo Jijini Arusha. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo na Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kwa pamoja wakifurahia mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Video unaowawezesha wanafunzi kuonana na kuzungumza na kuchangia masomo kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya mkoa huo wa Arusha, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo Julai 27, 2012 kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza    kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kuhusu matuzmi ya baadhi ya majengo yaliyopo katika Chuo hicho, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo Julai 27, 2012 kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.

Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Magazeti ya Ijumaa

Usalama Wa Taifa Wakanusha Kumtesa DR.Ulimboka

IDARA YA USALAMA WA TAIFA YAKANUSHA KUMTESA DR ULIMBOKA STEVEN

Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi.

Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wiki limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni
habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.

Idara inataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni za UZUSHI NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali
ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumiagazeti hilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.

Matukio yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.

Aidha, tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Idara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azima yetu ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na wanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.

Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM
26 Julai, 2012.

Magazeti Ya Leo Jumamosi 27th July 2012

Thursday, July 26, 2012

MH.SPIKA ANNE MAKINDA ASHEHEREKEA SIKU YA KUZALIWA

                                                                         Keki ilipowasili
                     Spika Anne Makinda akipokea keki kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Bunge.
                             Mhe. Spika Anne Makinda, Mb.akikata keki katika birthday yake .
                  Spika wa Bungbe Anne Makinda akikata keki tayari kwa kuila katika birthday yake

Hongera Mama Kwa Kufikisha miaka 60 na kustaaf

                             Pongezi za dhati Kabisa kwa uongozi mzima wa Arusha School
                                                              Mr &Mrs Lyimo
     Naona Mkuu wa shule anakuna kichwa tutapata wapi tena matron kama wewe mwenye maadili jamani
              Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Arusha School hakika mmeonesha mshikamano na upendo
                     Mama akiwa na Zawadi aliyopewa na wafanyakazi wa Arusha School
    Mamatron wakicheza na matron mwenzao ambae takrabani miaka arobaini waliishi pamoja kwa upendo
      Jamani ni huzuni ila ni furaha kukuaga Mamatron wakiwa wamekumbatiana kwa furaha na huzuni
                  Wafanyakazi wakatambua uwepo wa baba mchungaji hakika unastahili pongezi baba

                                                                 Hongera mama
                                                               Hongera mama
                                                                  Na saa ya Maakuli
                                                        Mama akichukua chakula
                                                                Baba akichukua chakula
                                               Mkuu wa shule Alichukua chakula
                       Mrs Christian wifi yangu mwenyewe mwingine photocopy mama
                          Mwana  blogger Mwenyewe Mwili haujengwi kwa matofali jamani
                                                         Kaka chukua msosi
                                             Mbunge wetu mtarajiwa big up mama
                        Matron wetu akitowa Nasahaa zake kwa wafanyakazi anao waaga
                                                                  Wakafungua Musiki
                                                                       Familia

                                                           Hongera mkuu wa shule
                                                  Tukabadilishana Mawazo na IT wangu Mtarajiwa
Kwa Niaba ya watoto natowa shukrani za dhati kwa wazazi wetu na uongozi mzima wa shule ya Arusha School kwa upendo mliotuonyesha tangu mama alipoaza kazi hadi Kustaafu mungu awazidishie mara mia tupo pamoja kwenye raha na shida.