Wednesday, February 18, 2015

hi nawatakia jumutano njema ya majivu

jamani nawatakia kwaresma njema na tumuombe mungu atusamehe makosa yetu leo tusisahau kwenda kanisani.

Monday, February 2, 2015

Bondia Francis Cheka amehukumiwa kwenda jela.

Bondia Francis Cheka leo February 2 2015 amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na faini ya Milioni moja laki sita kwa kosa la kumpiga mmoja kati ya wafanyakazi wake kwenye bar yake iliyopo Morogoro.

Muda mfupi uliopita Francis Cheka ameongea  na kusema ndio alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10 nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’

Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.

millardayo.com

Habari njema kuhusiana na majaribio chanjo ya Ebola…


Stori kuhusu ishu ya Ebola huenda ni moja ya story zilizochukua headlines kubwa kwa mwaka wote 2014, tangu iliporipotiwa kuibuka kwa maambukizi ya ugonjwa huo Afrika Magharibi mwanzo wa mwaka 2014.

Hii inaweza kuwa habari njema kwa Waafrika na dunia nzima kwa ujumla, taarifa iliyopo ni kwamba jaribio la kwanza la chanjo ya ugonjwa wa Ebola kutarajiwa kuanza kutumika Liberia wakati wowote kuanzia sasa.

Wataalamu wanatarajia zaidi ya watu 30,000 watajitokeza katika zoezi la majaribio hayo wakiwemo wahudumu wa afya.

Katika kipindi cha mwaka mmoja zaidi ya watu elfu tisini wamefariki kutokana na ugonjwa huo ambao uliandama zaidi Mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.

Toto langu kazini chezea precious wewee

Wednesday, December 31, 2014

TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI


 Katika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari "Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya". Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:

Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)

Taarifa za gazeti hilo zilieleza kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika uongozi wa Waziri Muhongo umekuwa ni wa kukatisha tamaa. Moja ya mifano iliyotolewa ni kuendelea kuwepo kwa wachimbaji madini wanaozidi kutorosha madini kwa nia ya kukwepa kodi.

DOKTA AONYA MIMBA YA AUNT!

TABIA za mitoko ya usiku matembezini, uvaaji viatu virefu na unywaji pombe unaofanywa na wamama wajawazito, kama alivyo sasa muigizaji Aunt Ezekiel, zimeelezewa kuwa si nzuri na zina uwezekano mkubwa wa kusababisha madhara kwa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.Akizungumza baada ya kuulizwa na gazeti hili juu ya mwenendo wa muigizaji Aunt Ezekiel ambaye mara kadhaa huonekana akiwa 'viwanja' usiku, daktari mtaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto, aliyejitambulisha kwa jina moja la Dokta Chale, alisema utokaji wa usiku na uvaaji wa viatu virefu unaweza kusababisha matatizo ya nyonga, shida wakati wa kujifungua, miguu kuuma na uvimbe kwenye vifundo vya miguu 'enka'.

Kuhusu unywaji pombe, Dokta Chale alisema endapo mama mjamzito atafanya tabia hiyo, ipo hatari ya uelewa wa mtoto katika ukuaji wake kuwa mdogo na pia kuchukua tabia zote za mama yake."Viatu virefu na mitoko ya usiku kwa mama mjamzito ina madhara makubwa sana kwani mtoto atakuwa na uelewa mdogo, yaani akili yake inakuwa haikui sawasawa, kifupi ana-adapti (kuiga) tabia zote za mama yake anaweza kuwa zezeta kama mama anatumia pombe," alisema.

Katika kudhihirisha kuwa ustaa ni kazi kubwa, licha ya ujauzito wake kuonekana mkubwa, Aunt Ezekiel amekuwa akijirusha kama kawaida sehemu mbalimbali nyakati za usiku huku wakati mwingine akiwa amevaa viatu virefu..

Globalpublishers