Soma hii habari kuhusu kauli ya Mbunge wa Korogwe Vijijini,Steven Ngonyani(Maji Marefu) na kujiuliza hivi baadhi ya hawa watu tunaowaita wawakilishi wetu huwa wanaropoka tu au wakiwa kule Bungeni wanasema kile ambacho wananchi wao wamewatuma au kile ambacho wanaamini kabisa kitasaidia wananchi wa jimbo wanaloliwakilisha?
Hivi kweli katika dunia ya leo ambapo wote tunaongelea habari za ukomeshwaji wa mateso(torture) dhidi ya binadamu, yupo Mbunge ambaye anaweza kusimama na kusema kipigo kama alichokipata Dr.Steven Ulimboka alistahili? Yaani kwa mwakilishi huyu,case closed,justice has been served! Mbaya zaidi Mbunge huyu hakutolewa Bungeni!
"Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu (pichani), leo amesema bungeni kuwa kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini.
Profesa Maji Marefu aliitoa kauli hiyo wakati akichangia hoja katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni Dodoma.
Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda alilazimika kuingilia kati kumzuia Profesa Maji Marefu asiendelee kutoa kauli hiyo kwani jambo la madaktari bado liko mahakamani."
Chazo: blog ya Michuzi
No comments:
Post a Comment