Friday, June 29, 2012
HIVI ULISIKIA ALICHOSEMA WAZIRI MKUU JANA BUNGENI? KUHUSU KUJIUZULU NA MGOMO WA MADAKTARI? CHOTE KIKO HAPA..
Jana ndio siku ambayo waziri mkuu Mizengo Pinda aliahidi kutoa jibu la serikali bungeni kuhusu itakachofanya kuhusu mgomo wa Madaktari.
Kuhusu kujiuzulu kutokana na mgomo wa sasa likiwa ni swali kutoka kwa mbunge Tundu Lisu wa Singida Mashariki amesema “yako mazingira unaweza ukawajibika kwa njia hiyo lakini sio lazima yakawa yoote na mimi sioni kama hili ni moja ya maeneo ambayo unaweza ukasema kistahiki hivi unaweza kufikia hatua hiyo, ninachokubali tu ni kwamba tatizo hili ni kweli ni la muda mrefu na nimefanya kila njia kujaribu kulitatua kwa kiasi kikubwa sana, inabidi tukubali kwamba bado lina changamoto nyingi kwa sababu ya mambo mengi tu ambayo yameingiliana na mgogoro wenyewe”
Freeman Mbowe kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni alisimama na kumuuliza Waziri Mkuu kwamba “ulitoa kauli ambayo kama mzazi au kama baba imetia hofu kubwa sana katika taifa pale ulipokua unazungumzia mgomo wa Madaktari na hatimae ukasema na LITAKALOKUWA NA LIWE, vilevile zilipatikana taarifa nyingine kwamba rais wa Madaktari ametekwa juzi usiku, ameteswa, kavunjwa meno, kango’lewa kucha.. unalieleza nini taifa kuhusu kauli yako ya LITAKALOKUA NA LIWE? na serikali inafanya nini cha ziada?
Hili ndio jibu alilotoa Waziri mkuu kwa Freeman Mbowe: “Kwanza nikiri kwamba ni kweli nilitamka hivyo jana lakini kilichokua kinanisumbua kichwani ni kwa sababu nilijua jambo hili liko mbele ya mahakama kuu, kuhusu yaliyompata Dr Ulimboka naonyesha masikitiko yangu juu ya jambo hili na ninamtakia kila la kheri na apone haraka”
Kuhusu alichoahidi kukiongea leo kuhusu Mgomo unaoendelea Waziri Mkuu amesema “tumezungumza na vyombo mbalimbali ili tuone katika mazingira tuliyonayo ni namna gani tutawahudumia wagonjwa, tumewaomba wenzetu wa LUGALO tutumie hospitali ile kuhakikisha wagonjwa hawakosi hiyo huduma, hata hospitali zake nyingine ndogo zote tumeamue tuzitumie kwa njia hiyo, lakini pia tumeona ni vizuri kama kutakua na madaktari wengine waliostaafu na wengine waliopo wizarani pale wote tumeomba sasa watafutiwe njia mbalimbali ili warudi waweze kutoa hiyo huduma kwa Watanzania”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment