Waziri
wa Fedha wa Tanzania,Dr.William Mgimwa akisoma Hotuba Ya Bajeti 2012
I UTANGULIZI:
1.
Mheshimiwa Spika, naomba
kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liweze kujadili na kupitisha makadirio ya
mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na
hotuba hii, nimewasilisha vitabu vinne vya Bajeti vinavyoelezea takwimu
mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinaelezea makisio ya mapato.
Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya kawaida
kwa Wizara, Idara zinazojitegemea; Taasisi na Wakala wa Serikali; cha Tatu
kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
na cha Nne kinaelezea makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa Wizara,
Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali; Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2012 ambao ni sehemu ya Bajeti hii.
Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2012 ambao ni sehemu ya Bajeti hii.
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nitumie fursa
hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kuniteua kuwa Waziri wa Fedha. Naahidi kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa kwa umakini na uaminifu mkubwa.
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kuniteua kuwa Waziri wa Fedha. Naahidi kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa kwa umakini na uaminifu mkubwa.
3.
Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza wafuatao kwa
kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa mawaziri kama ifuatavyo: Mhe. Prof. Sospeter
Mwijarubi Muhongo (Mb); Mhe. Mhandisi Christopher Kajoro Chiza (Mb); Mhe. Dkt.
Harrison George Mwakyembe (Mb); Mhe. Dkt. Fenella Ephraim Mukangara (Mb); Mhe.
Balozi Khamis Sued Kagasheki (Mb); Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb). Aidha,
napenda kuwapongeza wafuatao kwa kuteuliwa kuwa naibu mawaziri katika Wizara
mbalimbali, Mhe. Janet Zebedayo Mbene (Mb); Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb); Mhe.
Dkt. Seif Suleiman Rashid (Mb.); Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb.);
Mhe. January Yusuf Makamba (Mb.); Mhe. Dkt. Charles John Tizeba (Mb.);
Mhe. Amos Gabriel Makalla (Mb.); Mhe. Angela Jasmine Kairuki (Mb.); Mhe.
Stephen Julius Maselle (Mb.); na Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Satano Mahenge
(Mb). Kadhalika, nampongeza Mhe. James Mbatia (Mb) kwa kuteuliwa na Mhe. Rais
kuwa Mbunge.
4.
Mheshimiwa Spika, nawapongeza
pia, Mhe. Alhaji Adam Kimbisa (Mb.); Mhe. Shy Rose Banji (Mb.); Mhe. Abdulah
Alli Hassan Mwinyi (Mb); Mhe. Charles Makongoro Nyerere (Mb); Mhe. Dkt Twaha
Issa Taslima (Mb); Mhe. Nderkindo Perpetua Kessy (Mb); Mhe. Bernard Musomi
Murunyana (Mb); Mhe. Anjela Charles Kizigha (Mb.); Mhe. Maryam Ussi Yahaya
(Mb.), ambao wamechaguliwa kutuwakilisha kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Ni
matumaini yangu watatuwakilisha vyema kwa maslahi na manufaa ya Taifa letu.
5.
Mheshimiwa Spika,
maandalizi ya Bajeti hii yamehusisha wadau na Taasisi mbalimbali. Napenda
kuwashukuru walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha matayarisho
yake. Kwa namna ya pekee, ninaishukuru Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi chini
ya uenyekiti wa Mhe. Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi,
pamoja na kamati nyingine za kisekta kwa ushauri mzuri waliotoa wakati
wakichambua mapendekezo ya Bajeti hii. Aidha, ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge
wote kwa ushauri na mapendekezo yao ambayo yamezingatiwa katika Bajeti hii.
Read more: BongoCelebrity
No comments:
Post a Comment