Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akitoa
maelezo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA
Tanzania, uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar eSalaam. Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA
Mama Salma Kikwete. Mradi wa Fistula kwa mwaka inakadiriwa wastani wanawake wapya
2,500 hadi 3000 hupatwa na ugojwa huo wakati wanapojifungua. Kwa sasa wanawake
zaidi ya 31,000 inasemekana wanalo tatizo la Fistula hapa nchini, Hivyo Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito wakina mama wenye matatizo ya Fistula
kumuacha kujificha kwani unatibika .hivyo waende katika matibabu ambayo
hupatikana bure ktk hosp. ya CCBRT jijini DSM na hosp, ya Kilutheli
ya Selian.
Mama Kikwete akihutubia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa
Taasisi ya WAMA, akiwa amemshika mtoto mchanga baada ya kukabidhiwa na wazazi
wake baada ya ushuhuda walioutoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji
wa Matibabu ya Fistula- Tanzania. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya CCBRT,
Shuhuda wa ugonjwa wa FISTULA, Beatrice Mlunga (kulia) akitoa
ushuhuda wa matatizo aliyoyapata ya ugojwa Fistula wakati wa uzinduzi huo.
Kushoto ni mume wake, Hosea Sanga.
Mke wa Rais NaMwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (mwenye
miwani ) akiponyeza kitufe kuzindua kampeni hiyo.
Mjomba Mpoto akiwatumbuiza waalikwa wakati wa Uzinduzi.
No comments:
Post a Comment