Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema serikali imeagiza kuzingatiwa sheria ya vifo vyenye utata kwa kufanyika uchunguzi wa kina juu ya vifo hivyo ambapo pia amekanusha stori kwamba Tanzania imechafuka kwenye anga za kimataifa kutokana na matukio mbalimbali yaliyotokea.
Hii ni stori kutoka 104.4 Dodoma bungeni wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe kwenye maswali ya papo kwa papo ambapo ameamlfy kwamba kuwepo kwa hisia kuwa serikali inahusika katika mauaji ya raia sio sahihi na hata ishu ya Kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka Steven kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika sio vizuri ikatumiwa kama mfano.
Freeman Mbowe alimuuliza waziri mkuu kwamba “Mheshimiwa Waziri mkuu katika nchi yetu kwa muda mrefu sasa yamekuwepo mauaji mengi na baadhi ya vifo hivi vimekua na utata mkubwa na baadhi ya vifo hivi vimekua vikihisiwa kuhusisha vyombo vya dola kama vile jeshi la Polisi, lakini ni kweli kwamba hisia za dola kuhusika katika mateso na mauaji ya raia zimeendelea kuwepo na jinsi ninavyouliza swali hili sifa ya taifa letu iko mashakani katika anga za kimataifa kutokana na mateso ambayo yanaonekana yalikua na kusudio la mauaji ambayo alifanyiwa mwenyekiti wa madaktari Dr Steven Ulimboka”
Alichojibu Waziri mkuu ni hiki….. “Sio kweli kwamba jina la nchi yetu limechafuka, kuchafuka sana kwa lipi? ukisema hivyo ni lazima vilevile uwepo ushahidi wa dhati unaoonyesha kwamba ni kweli serikali inahusika, sasa umetumia mfano wa Ulimboka… sio mfano mzuri, we huna ushahidi kama ni serikali imefanya hivyo na hakuna mpaka sasa anaeweza kusema ana ushahidi huo, ndio maana tulisema mara ya mwisho kwamba ni vizuri jambo hili likafanyiwa uchunguzi wa kina ili tujue kilichotokea hasa ni kitu gani”
Kwa kumalizia kumjibu Freeman Mbowe, Waziri mkuu amesema “hainiingii kichwani hata kidogo kwa mtu ambae tumekua tunafanya nae kazi muda wote alafu sisi hao hao tuchukue hatua tena ya kutaka kwenda kumuadhibu kwa namna iliyotokea, haiingii kichwani”
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Waziri Mkuu amesema serikali imefanya jitihada kubwa katika kuwekeza kwenye sekta ya Afya hasa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili ambako hivi karibuni taasisi ya moyo itazinduliwa, ameamplfy pia kwamba hatua nyingine ni kuipandisha hadhi hospitali ya Jeshi Lugalo ili kuwa hospitali ya rufaa.
No comments:
Post a Comment