Sunday, August 5, 2012

AJALI MBAYA YA MALORI YAUA WANNE KITONGA IRINGA

 
 Wananchi mbali mbali pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa (hayupo Pichani) MOhamed Mpinga wakitazama malori mawili yaliyogongana katika mteremko wa Kitonga Iringa usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu wanne baada ya kutumbukia katika korongo
 Gari ya kampuni ya Asas Iringa ikijaribu kutoa msaada wa kuvuta malori yaliyogongana ili kutoa maiti iliyonabanwa na malori hayo
                        Mwili wa dereva wa lori ukiwa umebanwa katika eneo hilo la tukio
      Askari polisi na wananchi wakitazama moja kati ya maiti zilizo naswa katika mabaki ya malori hayo
                    Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga akiwa eneo la tukio
 Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga akipandisha mlima kutoka katika korongo la mlima Kitonga Iringa akitoka kushuhudia ajali mbaya ya malori mawili yaliyogongana na kutumbukia korongoni na kupelekea vifo vya watu wanne papo hapo usiku wa kuamkia leo
                      Hivi ndivyo malori hayo yalivyogangana eneo hilo la Kitonga leo
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga (kushoto) akiwa eneo la ajali mlima Kitonga leo

HUKU mkoa wa Iringa ukiwa umepewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa mwaka huu ,mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda ashuhudia ajali mbaya iliyopelekea vifo vya watu wanne kufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam .

Hata hivyo dereva wa lori bovu ambalo lilikuwa limeegeshwa eneo hilo alipona katika ajali hiyo .

Akizungumza katika eneo la ajali mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga alisema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la scania ambalo lilikuwa na mali mbali mbali za dukani lilikuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo kugongwa na lori lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania ambalo lilikuwa limebeba shaba kuligonga lori lililokuwa limeegesha kando ya barabara hiyo.

Mpinga alisema kuwa katika ajali hiyo watu wanne walikufa papo hapo na mmoja ambaye ni kijana alijeruhiwa vibaya na kuwa miongoni mwa waliokufa ni pamoja na mwanamke mmoja ambaye inasadikika ni mkazi wa wilaya ya kilolo aliyekuwa amepanda katika lori hilo .

Alisema kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na utingo wa lori ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara hiyo ambalo lilikuwa limebeba mali za dukani ambaye alikuwa nje ya lori hilo akifanya mawasiliano ya simu na mwenzake na hivyo kugongwa na lori hilo la Shaba ambalo breck zilionyesha kuwa na matatizo.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na ajali hiyo kutokea Agosti 4 majira ya jioni ila zoezi la utoaji wa maiti ya dereva wa lori hilo lenye shaba bado ni gumu kutokana na mwili wa dereva huyo kubanwa vibaya ya tela la lori hilo lenye shaba .

Alisema kuwa kabla ya tela hilo lenye shaba kufunika kibini ya lori hilo kebini hiyo ilikatika na kutangulia korongoni na baada ya hapo tela lenye shaba kufuata nyuma na kutua juu ya kibini hiyo.

kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo imetokea wakati mkoa wa Iringa unataraji kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama ambayo kitaifa itafanyika katika mkoa wa Iringa huku akiwataka madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani kama njia ya kuepuka ajali kama hizo.

Aidha alisema kuwa kutokana na eneo hilo la mlima wa Kitonga kuendelea kuwa na eneo maarufu kwa ajili tayari mkakati umewekwa kwa ajili ya kuongeza ulinzi en eo hilo pamoja na kufanya doria za mara kwa mara za miguu ya magari kwa askari wa usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali katika eneo hilo.

Alisema kuanzia sasa askari wa usalama barabara watawekwa eneo hilo ili kuweza kukagua magari yote ya abiria na mizigo ili kabla ya kushuka mteremko huo kuwa na uhakika wa breck kama njia ya kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ajali mbaya katika mteremko huo.

No comments: